Nahodha wa timu ya Liverpool Steven Gerrard amemshutumu mchezaji mwenzake Mario Balotelli kwa kuonyesha utovu wa nidhamu pale alipolazimisha apige mkwaju wa penalti badala ya Jordan Henderson aliyekuwa tayari anakwenda kupiga adhabu hiyo dhidi ya timu ya Besiktas ya Uturuki.
Balotelli alifunga penalti hiyo na kuiwezesha Liverpool
kuibuka washindi wa bao 1-0 katika mchezo wa ligi ya Uropa unaozishirikisha
timu 32 uliochezwa Alhamisi katika uwanja wa Anfield.
Hali
hiyo ilijitokeza baada ya kushindwa kuelewana na nahodha wa mchezo huo
Henderson na Daniel Sturridge juu ya nani abebe jukumu la kupiga penalti
hiyo.
Gerrard amesema: "Henderson ni nahodha na Balotelli kwa kiasi fulani alionyesha kumkosea adabu katika hali hiyo."
Gerrard
ambaye kwa sasa ni majeruhi, alikuwa mchambuzi katika matangazo ya
mchezo huo kwenye televisheni ya ITV ya nchini Uingereza.
Steven Gerrard nahodha wa Liverpool
Gerrard
amesema kuwa Balotelli alikuwa "kwa kiasi fulani kakosea" baada ya
mchezaji huyo wa kimataifa wa Italia kumnyang'anya mpira Henderson,
ambaye alikuwa amejitayarisha kupiga penalti hiyo.
Henderson
alikuwa nahodha wa Liverpool dhidi ya Besiktas, na Gerrard anaamini
angekuwepo katika mchezo huo angepiga penalti hiyo.
"Sheria
ni sheria," amesema. "pongezi kwa Mario, amefunga, lakini si vizuri
kuona wachezaji wakibishana. Nafikiri Jordan alilichukua suala hilo
vizuri."
Kocha wa Liverpool Brendan Rod
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon