PENZI LA DADA...........BOOK 2-32
Mtunzi...................Chriss
.....................trisha!!!!!
JOHN!!!
trisha nna matatizo makubwa sana ni kama bahati leo umefika hapa"!
john najua yote yaliyokupata"
trisha ! wwe umejuaje!?
John Boss wangu yupo tayari kukusaidia"
kunisaidia! kwani Boss wako ni nani na kanijuaje!?
mimi nilikua nafanya kazi pale kwaajili kuchunnguza biashara za pale na sisi ndio wahusika wa zile mali zilizopotea!
kwahyo unataka kuniambia Trisha wewe ndio uliyesababisha mimi nikamatwe"!?
John ile ilitokea kama bahati baya na ndio mana nilimuomba Boss akusaidie"!
atanisaidia vipi na umesema nyinyi ndio wahusika"!?
John nisikilize mimi utapata msaada"

haya niambie utanisaidia vipi Trisha"?
unachotakiwa kufanya John ukifika mahakamani ukubali kua wewe ndio mhusika wa wizi wazile thamni zilizoibiwa"!
sikutaka hata amalizie nikamuuliza sasa Trisha huko ndiko kunisaidia au kuniangamiza"
John wewe ndio uchague unataka nini mana ukikubali mahakamani kua wewe ndio mhusika sisi tutakusaidia utoroke jela na tutakupeleka mahali popote upatakapo na hata kama ukikataa wewe sio mhusika mimi ndio msaidizi wako wa mwisho nitakubali kweeli uliiba mana mimi ndio shahidi wa kesi yako?
baada ya kusikia maneno hayo nililia sana mana nilijua sasa hatma yangu ipo mikononi kwa mwanamke ambae nilikua namuona kama mwanamke mzuri lakini kumbe ni jambazi na katili
John hata ukilia haitakusaidia"!
lakini kwanini mimi Trisha"!?
John tuseme tu! hii imekuangukia ww safari hii na tamaa zako za penzi ndiio zimekuponza na John kaa ukijua wewe sasa unatafutwa karibia dunia nzima kwani malikia mwenyew kasema atakayewezesha mkufu wake kupatikana atampa zawadi ya ardhi yenye mafuta katika milki yake ya nchi ya wales kwahyo ni wazi unahitaji kujificha na Boss wangu yupo tayari kukusaidia"!
niliinuka sikujali hata maumivu niliyokua nayo kwa hasira nikamkaba Trisha na kumwambia nakuua mimi siwezi kukubali uniharibie maisha yangu lakini wakati nimemkaba kumbe yeye alikua na silaha ya kupiga shoti akanipiga shoti nikaanza kujikunja nikadondoka hadi chini kisha! Trisha hakuacha kunipiga shoti huku akiendelea kunitisha kua endapo ntamueleza mtu yeyote basi Coleen na familia yangu yote watapoteza maisha !
nililia sana kwa uchungu kwani nilijua tamaa yangu ya penzi sasa inanileta doa katika maisha yangu!
wakati Trisha anaondoka nikamuuliza lakini kwanini mimi?
John hilo swali halitokusaidia"!
niliendelea kulia sana huku nikiwaza na kuwazua chaguo sahihi kati ya yale mawili siku hiyo yte ilikua mbaya kwangu na kibaya zaidi ni mkwara walioniwekea kua endapo nitasema watawaua watoto wa Coleen na Coleen mwenyewe sikutaka kucheza karata na maisha ya watu niwathaminio kuliko kitu chochote duniani " kwahyo niliapa kua sitamwambia mtu yeyote kuhusu jambo lile na mimi mwenyew niliamua kuendelea kufikiria nini la kufanya kwani ukweli ni kwamba sikua na chaguo lingine zaidi ya lile Malkia wa Wales ni mtu anayethaminiwa sana duniani mkufu wake ambao umepotea ni kitu ambacho matajiri wapo tayari kulipia gharama yeyote ili aupate kwani mwenyew ameahidi atakayewezesha kupatikani kwa mkufu wake ambao ni mali aliyorithishwa na wazazi wake atampa ardhi katika sehemu yenye utajiri wa mafuta milki yake ya nchi ya wales zawadi hiyo haikua ndogo watu wote matajiri duniani wanaitamani kwahyo ilikua wazi nitakua natafutwa sana watu wengi waliamini mimi ndio mhusika kwani mkanda wa video ulikua ni ushahidi mkubwa uliopatikana katika kesi hiyo na ule ushahidi ulikua unanilenga mimi kwa asilimia kubwa,!
hii iliashiria nilikua nahitaji kuhama nchi na kama Trisha alivyosema Boss wake yupo tayari kunihamisha nchi ila kwa sharti la kua nikubali mimi ndiye mhusika"
je JOHN ATAKUBALI SHARTI LA KUKUBALI KUA YEYE NDIYE
SAFARI YANGU.....
Mtunzi: Father faith
Sehemu ya 6
Endelea.......Baada ya kusikia polisi wapo nje na wanataka kuingia ndani kwa ajiri ya ukaguzi wa nyumba nzima nilihisi kuchanganyikiwa na kuona kana kwamba ndo naenda kuozea gerezani tena nikiwa ugenini. sehemu ambayo sina ndugu wala rafiki wa karibu na wakati hayo yote yanatokea Madam alikuwa hayupo ameshaenda ofisini lkn nikiwa katika hali ya kujiuliza nini nitafanya huku nikichungulia dirishani ili kujua kinachoendelea kule upande wa getini, ghafla nikaona gari aina ya Range ikiwa imesimama kwa nje ya geti wakati huo wale polisi ndo walikuwa wanajiandaa tayari kuingia ndani na kukamilisha kile kilicho waleta kumbe kwenye ile gari alikuwa ni madam ambae alirudi wakati ule kutokana na kusahau Laptop yake ndani kwani mara nyingi huwa anarudi nayo na kumalizia kazi ndogondogo za ofisi akiwa nyumbani lkn alishangaa kukuta wale polisi pale nje ndipo aliposhuka na kuwauliza kama kuna tatizo lolote kwani hakutegemea kukuta polisi pale ndipo askari mmoja mwenye cheo cha Inspector alipomjibu kwa kumwambia kama kunatukio limetokea la kupotea kwa Askari wawili waliokuwa wakiwakimbiza watu ambao inasemekana walikuwa wazamiaji waliongia nchini wakitokea Morocco lkn kwa bahati nzuri walikamatwa lkn wakati wakiwa njiani kuwapeleka sehemu inayohusika ndipo walipofika maeneo ya msitu wa asili waliruka kutoka kwenye gari na kuanza kukimbia lkn wawili kati yao wali u.....akasita kidogo yule Inspector na kumalizia kwa kusema walikamatwa hakutaka kutamka kama waliuwawa. Ndipo madam baada ya kuona hivyo akaona kama hana jinsi isipokuwa kutumia umatemate ili kuwaweka sawa hivyo alichofanya nikuingia nao ndani na kuwaacha wale maafande wakague upande ule wa chini na yeye moja kwa moja akaingia chumbani na kutoka na bahasha iliyokuwa na zaidi ya dola 20000 na kumkabidhi yule inspector na kumuomba ule ukaguzi uishie pale na wao wachukue zile pesa waondoke haikuwa kazi ngumu sana kuwashawishi kutokana na mdololo wa uchumi ktk nchi nyingi za ulaya hali iliyosabisha ktk njanja nyingi za serikali kuyumba hivyo kushindwa kabisa kulipa wafanyakazi wao kwa wakati. Ndipo yule Inspector alipo waamuru wale polisi wengine waliokuwa chini yake kuondoka pale ndani mara moja. Madam alikuwa na wasiwasi sana nadhani kuliko hata mm kwani endapo mm ningekamatwa tena nikiwa ndani ya nyumba yake ningeweza kusabisha matatizo kwake na kwa familia ndo mana akaona ni bora kutumia rushwa ili kujiokoa yy mwenyewe na mm pia.Lkn Kwangu mm nilidhani ndo ungekuwa mwisho wangu wa mm kuendelea kukaa pale ndipo nikiwa ktk hali ya kufikiria mustakabari mzima maisha yangu utakuwaje!! Wa mm kuendelea kukaa pale hata kama ni kwa mda nikiwa ktk hali hiyo ya kujiuliza ndipo nilipomuona Madam akiingia pale chumbani nilipo na kuja moja kwa moja mahala ambapo mm nimekaa na kuniuliza kama niliyaona yale yaliyotokea ndipo nilipo mwambia kama niliyaona yote na kumshukuru kwa mara nyingine kwa kuokoa maisha yangu na ndoto zangu kwa ujumla kwani kwa hakika bila msaada wake na huruma yake kwangu pamoja ya kuwa alinigonga na gari yake lkn msaada wake ulikuwa ni msaada mkubwa sana kwangu. Ndipo aliposema yakuwa anahitaji kujua kila kitu kuhusu mm ili aweze kunisaidia kwani bila hivyo atashindwa kwani ninaweza kuhatarisha usalama wa maisha yake na mali zake kwa ujumla...Ndipo nami bila kusitasita wala kumung'unya maneno ilibidi kumsimulia A to z ya maisha yangu hadi pale yeye alinikuta****Je nn ambacho Arkadir kilimkuta hadi akawa anatafutwa Morocco?Usikose sehemu ya 7.Pa1
>>>> SOMO LA LEO 16 <<<<
Kijana mmoja alienda omba kaZi katika nafasi ya juu kabisa ya umeneja katika kampuni fulani , alifanikiwa pita kila hatua iliyo itajika ili apate kazi , hatua ya mwisho kabisa alikuatana na director kwa ajiri ya interview ya mwisho kabisaa .
Director aliweza kugundua kua CV ya jamaa ilikua kali sana masomo kalibia yote alikua na "A" , alimuuliza kijana huyo je " kijana uliwahi kupata scholarship mahali ya shule ?"
Jamaa akajibu "apana "
"Nani aliekulipia shule mpaka umefika hapo ulipo soma elimu hii ? Au baba yako mzazi nn ?"
Kijana akajibu "hapana baba yangu alikufa ningali mdogo sana , alie nilipia alikua MAMA yangu mzazi "
Director akauliza "mama yako alifanya kazi wapi kijana ?"
Kijana "mama yangu alikua DOBI na pia alikua MSUSI maarufu sana mtaani kwetu na ndio kazi zake"
Director alimuomba kijana amuoneshe viganja vyake , kijana akafanya hivyo , kijana alimuonesha director viganja vyenye ngozi laini na nyororo visivyo na mkwaruzo hata mmoja .
Director alisema " kijana toka umezaliwa umewahi kumsaidia MAMA yako kufua nguo ?
Kijana alijibu " hapana sijawahi toka nizaliwe MAMA yangu alipenda mie niwe nasoma yeye hufua hadi nguo zangu mpaka leo hii , yeye hupenda mie nijisomee mda wote vitabu vyangu vya shule , ila kiukweli MAMA yangu yeye hufua kwa haraka kuliko mie "
Director alinena nae tena na kumwambia " Nina ombi moja kwako kijana , nenda nyumbani leo naomba umuombe mama yako mikono yake kisha uioshe ,kisha urudi hapa tuendelee na interview sawa "
Kijana aliona nafasi ya kupata kaZi ya umeneja katika kampuni ile ilikua kubwa sababu interview haikua ngumu, alipo rudi nyumbani ,alimuomba mama yake nafasi amsafishe mikono kama alivyoa agiZwa , MAMA yake alishituka na kuona ni kitendo cha ajabu kuwahi fanyiwa na mwanae kunawishwa mikono , alipata mawazo tofauti lakini alimpa mikono mwanae amnawishe .
Kijana alisafisha mikono ya MAMA yake taratibu , machozii yalianza mdodoka taratibu kadiri alivyo endelea kuosha mikono ya MAMA yake huyo ,ilikua ni mara yake ya kwAnza kushika mikono ya mama yake na kugundua imepasuka yaani ilikua na MACHACHA na ina mikwaruzo mingingi na haikuwa nyororo kama yakwake, na alivyo zidi kushangaa na kumbonyeza bonyeza mikono ile mama yake alitoa sauti kama mtu alie shikwa kidonda kibichi .
Ilikua ni mara ya kwanza kijana huyo kutambua kuwa mikono hiyo miwili ilifua nguo na kusuka kila siku ili aweze pata japo fedha za kulipa ada ya shule .mpasuko ya ngozi ngumu iliyo katika viganja vya mama yake ilikua ndio jasho ama gharama mama yake alizopitia ili yeye aweze soma , na aweze kuwa na maisha mazuri siku za mbeleni .
Baada ya kumaliza kuosha mikono ya mama yake , kijana alimuomba mama yake nguo na kumfulia nguo zake zote zilizo kuwepo siku hiyo.
Siku hiyo MAMA na mwana waliongea kwa mda mrefu jambo ambalo sila kawaida kwa maisha yao ya kila siku .
Siku iliyo fuata asubuhi ,kijanaa alienda katika shirika lile na kuomba kuongea na DIRECTOR .
Director aligundua machozi yakimtoka kijana yule kila akimuangalia .
Director alimua kumuuliza kijana yule "waweza nambia unejifunza nini kutokana ma maagizo niliyo kupa siku ya jana ?"
Kijana akajibu "nilipokua namuosha MAMA yangu mzazi ,mikono niliamua kufulia nguo zote alizokuwa nazo siku hiyo "
"Kwa sasa ninajua ninaitaji kumshukuru kwa namna gani kwa yote alo nifanyia maishani mwangu ,bila yeye nisinge kua hapa nilipo ,kwa kumsaidia mama yangu mzazi ninatambua nijinsi gani ilivyo ngumu kufanikisha jambo mwenyewe ,na natambua mchango wa kusaidiana katika familia hizi tuishizo ama tunazo tokea .
Director alisema " hiki ndio ninachohitaji /nikitaftacho kutoka kwa manager wa kampuni hii ,ninataka kumuajiri mtu ambae atatambua umuhimu wa msaada wautoao wengine katika kampuni ,mtu ataetambua nijinsi gani wenzie wanaangaika kila siku ili kukamilisha kazi fulani, pia MTU ambae hatoweka PESA mbele kama kitu pekee muhimu MAISHANI KWAKE !"
"KUANZIA SASA WEWE UMESHA AJIRIWA KATIKA KAMPUNI HII "
Kijana huyu alifanya kaZi kwa bidii ,aliheshimika kwa watu wa kila lika ofisini hapo ,watu walifanya kazi kwa umoja na kuheshimiana sana na mwisho wa siku kampuni iliendeleaa kukuaa sanaa na kutengeneza faida kubwa kila siku !!
SOMO
Mtoto aliekulia katika mazingira mazuri nyumbani na kupata kila atakacho , husahau na kupuuza nguvu na jitihada zilizofanywa na wazazi wake mpaka kufikia hApo walipo,mtoto hufikilia kuwa anatakiwa kusikilizwa kila atakacho au asemacho na siku zote huwa na dhana za kuwa anahaki ya kupata kila atakacho na atajiweka yeye mbele au wa kwanza wengine watafatia ,na akianza kazi yeye yeye huamini kila mtu anatakiwa amsikilize kwakua yeye ndio bosi na akifanikiwa kuwa manager hawezi kujua hata siku moja shida na tabu wapatazo wafanyakazi wake na atawalaumu na kuwagombeza kila siku wakikosea .
Watu wa namna hii huwa ni waZuri kielimu au kimasomo , wanaweza leta mafanikio ktk kampuni ,lakini hawato ridhika watawafanyisha kazi watu hadi chuki zianze ndani ya kampuni ,kama wewe ni aina hii ya mzazi ,unamuachia mwanao pasipo kumkanya na kumpa malezi mazuri ,je tunaonesha mapenzi kwa watoto wetu au tuna waharibu watoto ?
Waweza waacha watoto wako waishi ktk jumba kubwa ,wale chakula kizuri ,wacheze game ,wakifunze kupigaa gitaa ,angalia movie kwenye tv kubwaa ,lakini wakati unaangaika na maisha wafundishe na ujumuike nao mda mwingine ile nao waone shida uipatayo mazazi ,wakimalza kula waache waoshe vyombo na kaka na dada zao,sio kwamba hauna pesa ya kumuajiri house girl bali unatakiwa uwapende kwa njia sahihi ,lengo waelewe maisha hata kama wazazi wao ni matajiri kiasi gani ,kitu muhimu ni MTOTO wako kujifunza kushukuru na kutambua umuhimu na mchango watu na vile vile wanao mzunguka katika jamii ktk maisha ya kila siku na pia kujua ugumu wa wakazi , ili wajifunze kuishi na kufanya kazi kwa kushirikiana na wengine ili kazi ifanyike kwa ufanisi na umoja .
Je umeipenda ? Jaribu kuifoward msg hii kwa ku "SHARE " kwa watu wengi ,yaweza badilisha maisha ya mbele ya MTOTO

NYAYO ZA KUZIMU--11
"Inatubidi tusali mama Kadogo,mungu awe nasi na atushike mkono,atuongoze kuuvuka huu mto,na pia milima ile....na hata mmoja wetu asipofanikiwa isiwe mwisho wa mapambano yetu.umenisikia mama Kadogo?"
sura yenye msisitizo isiyotania ya mzee Otongo iliyatamka yale maneno.
"sawa mzee Otongo,inatubidi tupigane mpaka tone la mwisho la damu yetu,inabidi tufe tukijaribu"
alieleza mama Kadogo huku chozi likimlengalenga.
Aliyatupia macho ya huruma kwa mwanae,akachuchumaa akambusu kwenye paji la uso kisha aliinuka na kusema
"sasa tunaweza kuvuka.."
akamueka mwanae mgongoni,akaanza kusogelea maji ya mtoni taratibu huku akitanguliwa na mzee Otongo.
Mto Inguvai hauna daraja la kumuwezesha mtu kuvuka kwa urahisi,ni utashi wa mtu tu ndio unaotakiwa ili aweze kurukia mawe yaliyokuwepo pale kwa ajili ya kuikuta ng'ambo,ilimuwia vigumu sana mama Kadogo kurukia yale mawe kwani ukiachana na lile giza la ule muda bado alikua na mtoto mgongoni,walisogea hatua mbili tatu huku moyo wa kila mtu ukidunda kwa uoga na tumbo la kila mtu likisokota kwa uoga pia,mawe waliyokua wanayakanyaga yalikua yameshika utelezi hivyo ilihitaji uangalifu mkubwa na bado miguu yao iliyo peku ilikua inapitiwapitiwa na maji kitu kilichoashiria ya kwamba maji ni mengi kiasi cha kukaribia kufunika yale mawe yatumiwayo kama kivushio,hakukua na muda wa kutosha wa kuangalia nyuma,kila mtu aliyatoa macho kwa kiasi kikubwa ili yapambane hata kidogo na lile giza lililopo ili apaone pa kuutuliza mguu wake,walizidi kusogea na mwendo wao wa kinyonga na ilibakia kama mawe matano tu ili waweze kupita kile kizuizi,ghafla sauti kubwa ya mlio wa pembe la ng'ombe iliskika!!
Haraka kwa uoga mama Kadogo aligeuka nyuma kabla sauti ya mzee Otongo kufika masikioni mwake ya kwamba hatakiwi kugeuka!!
Mguu wake wa kulia ulio mbele uliteleza na kumfanya aifungue mikono yake kwa ajili ya tahadhari ya anapodondokea na kumuacha Kadogo aliekua kambeba mgongoni akidondoka kwa urahisi!!!
Mikono yake miwili ilishikilia mawe kwa nguvu na kumfanya abakie salama kwa kutopelekwa na maji ila mwanae Kadogo ambaye kamwili kake hakakutosha uzito kushindana na ile nguvu ya yale maji alibebwa kama kikaratasi akimuacha mamaye akilia kwa uchungu bila msaada wowote!!
Mzee Otongo ilimbidi arudi nyuma kitaratibu,alishika mikono ya mama Kadogo iliyoanza kuzidiwa nguvu na kuanza kumvuta kwa lengo la kumuondoa kwenye yale maji yenye kasi kubwa!!
"mama Kadogo jitaahiiidiiiiiiii!!!!.."
"mzee Otongo niache tu nife! Mwanangu jamani!!!!!"
"mama Kadogo hatuna muda wa kupotezaaa!!!!..
Tafadhali jitahidi utoke kwenye hayo maji nguvu inaniishiaaa!!!!!"
"mwanangu Kadogo jamaniii!!!"
"mama Kadogooo!!!...tafadhali nadhani unakumbuka nilivyokuambia kabla hatujavuka..tafadhali jitahidi utoke,tafadhali nguvu zinaniiiishaa!!!"
kwa nguvu aliropoka huku akikunja sura!
* * * *
upande wa pili wa shilingi jeshi la 666 lilikusanyika,ile mbiu ya pembe la ng'ombe iliyopigwa ilikua ni ishara ya kwamba wanaitwa,walisimama kwa utulivu na usikivu,na tahamaki ndani ya jeshi hilo mama Utopi alikuwepo!!..na si tu huyo hata mama Marinda na Vero!!...walishapigwa chapa,hivyo walishakua chini ya utawala wa Chernobog!!
Mzee mmoja asie mfupi wala mrefu yani saizi ya kati alisimama mbele yao,mkononi alishika fimbo yenye alama ya nyota nyekundu na kimavazi alinawirishwa kwa rangi nyeusi na nyeupe,macho mekundu na lips zake pana ziliönyesha ana kabiliwa na jambo,bugudha na hasira zilionekana kumteka!!
Kabla ya kufungua mdomo na kunena jeshi la 666 liliinamisha vichwa na kudhihirisha ya kwamba alie mbele ni mkubwa wao,
"ni nyota ndio iliyotuita!
Ni kwasababu ya nyota tupo hapa!!
Nyota nyingine imechomoza angani,nyota itishiayo nyota ya CHERÖBOG!!!..nyota imaanishayo ya kwamba kuna mtoto anazaliwa,nyota imaanishayo hatari kwa utawala wa giza,nyota itakayoamsha tena Jua lililopotea,nyota itishiayo makazi ya KUZIMU duniani!!!
Hakikisheni huyo mtoto haponi! HAKIKISHENI MNAMTOKOMEZA KABLA JUA HALIJACHOZA TENA!!! HAKIKISHENI MNAMMALIZA HARAKA IWEZEKANAVYO!!!"
"Ameen!!"
waliitikia na kutoweka haraka kwa kasi wakielekea kule mtoni walipo wa kina mama Kadogo na mzee Otongo!!
Watapona kweli kwa ile kasi? Na ni nani atakua wa kwanza kumchukua yule mtoto alie katika kijiji cha Utowele?
Vita kati ya giza na mwanga ndio inaanza??
UsIKOSE!!

NYAYO ZA KUZIMU--27.
(muda usiosogea)
Young Chriss
waliwadadavulia na kuwanyumbulia wanakijiji kwa undani tangu walipotokea na nini kimewaleta hasa.Maneno na maelezo yaliyotolewa na wakina mzee Otongo yalionekana kuwatisha zaidi wanakijiji,habari za jeshi la 666 zilikua ni za kuogofya na zenye kutaka ujasiri kuzisikia,hakukua na jinsi ilibidi waambiane ili wapate pa kuanzia,elimu hasa iliyokua inatolewa juu ya kiendeleacho ndicho kilikua cha kwanza kisha hayo mengine yachukue nafasi,zoezi lilifanikiwa na kumalizika salama huku likianzisha ukurasa mpya wa maisha yao ambao walikua hawajautambua,nia na nguvu yote ya wanakijiji ilielekezwa juu ya kumlinda yule mtoto aliezaliwa na mengine pia kama watakavyoelekezwa kufanya na viongozi wao waliowateua ambao ni Mzee Patili,mama Kadogo na mzee Otongo,hakukuwa na ubishani tena wala minong'ono isiyo na msingi,sasa kila tendo lililochukua nafasi lilikua ni maelekezo dhabiti toka kwa viongozi wao,hakuna alietia dosari.
Mzee Patili aliwataka wanakijiji wajipange mistari miwili ya kijinsia,bila kuchelewa wakajipanga,alivichukua vibuyu vyake na kimoja akamkabidhi mama Kadogo kisha akampa maelezo madogo tu yaliyofanikisha kumjuza kiendeleacho,zoezi la kuwapaka wanakijiji dawa usoni na mikononi kwa lengo kuu la kudhoofisha nguvu za adui wao lilichukua nafasi,mzee Patili akiwa anapakaa mstari wa wanaume na wavulana huku mama Kadogo akiwa anashughulika kwenye mstari wa wanawake na wasichana,idadi ya wanakijiji iliyokuwepo haikuendana na kiasi cha dawa husika hivyo ilipelea,watu kama ishirini hawakua wamepakwa dawa kitu kilichompa maswali mzee Patili juu ya nini hasa cha kufanya,baada ya kufikiria kidogo aliwachagua wanaume wawili (mrisho na tabwe) kisha akawaagiza waende nyumbani kwake kwa lengo la kuchukua dawa ili apate malizia waliobaki,ujasiri waliopewa na dawa walizopakwa ziliwafanya wasijifikirie mara mbilimbili,haraka walijiondoa lile eneo na kueleke walipotumwa.
Wakati hayo yote yanachukua nafasi lile jibaba linyongaji lilikua likishuhudia,kwa mbali lilijificha kwenye mapori ila macho yake mekundu makubwa yalimfanya aone vizuri kilichokua kinafanyika,hakua peke yake kwa sasa hivi kama ilivyokua,pembezoni yake alikuwepo mwanamke mmoja mwenye macho ya paka na ulimi mwekundu!!! Alijivika kaniki nyeusi na kiremba chekundu kilichositiri mapembe yake vizuri,ngozi yake ilikua na rangi ya kijivu na masikio yake yalikua marefu ilihali na kucha za mkononi,sasa walikua wawili kwa idadi,jeshi la 666 liliongeza mashambulizi!!! Wanakijiji watahimili hili??
Lile pande la mtu jeusi na yule mwanamke mithili ya paka walitabasamu na kuruhusu meno yao ya kutisha kuonekana,walipeana ishara,wakashika njia na kuelekea kule wale wanaume walipotumwa,yani kwa mzee Patili kwa lengo la kuzuia zoezi la uletaji dawa,lile Pande la mtu mkononi lilishikilia kamba nyekundu kama ilivyokawaida yake na yule mdada mithili ya paka akiwa na kisu kirefu!!!
Matamanio yao ya kuua bila kuchelewa na kufanikisha lengo lao yaliwafanya wajione wanachelewa kwa kutembea,hivyo walianza kukimbia huku macho wakiwa wameyatupia mbele!!
* * * * * * *
mrisho na mwenzake walishafika eneo husika,walikua ndani ya kijumba cha mzee Patili wakifanya jitihada za kusaka dawa waliyotumwa,uwepo wa dawa nyingi mule ndani ulifanya zoezi liwe gumu kwani kila dawa waliyoipata walipoinusa waligundua sio yenyewe,ilichukua kama muda wa dakika saba mpaka walipoitia mkononi iliyolengwa,waliangaliana kwa tabasamu kisha wakaelekea mlangoni,Mrisho aliunyoosha mkono wake na kuuvuta mlango,mlango ukagoma kufunguka!! Alizidi kutumia nguvu zaidi lakini bado matokeo yakawa yaleyale,mlango uligoma kabisa kufunguka!!! Ikabidi amuachie Tabwe nae ajaribu lile zoezi,hakuna aliefanikiwa,bado hawakuweza kuufungua,hofu ilianza kuchochewa mioyoni mwao,wakaangaliana kwa uoga huku kajasho kakitirika,Tabwe huku akitetemeka akasema..
"Mrisho..tunakufa...!!"
Mrisho akameza mate,moyo ulikua unampwitampwita na macho yakimtoka,alipata wazo kichwani haraka akamwambia mwenzie
"Tabwe...tu..tu..tuvunje mlango!!!"
Tabwe alionekana kukubaliana na hilo wazo lililoonekana ni pekee kwa ukombozi wao,bila kuchelewa harakati za uvunjifu zikaanza kikamilifu kwa kutumia mateke,hawakua na habari ya kuwa lile jibaba linyongaji na yule mdada mithili ya paka walikua kwa nje wakiwasubiri kwa hamu zote ili kuongeza idadi ya waliokwenda na maji na kusafisha njia ya kufanikisha lengo lao,puh!! Mlango ukatupwa kule na nguvu ya teke zito la wakina Mrisho!! wakatoka nje,he!!! hawakuamini walichokiona!! Kitendo cha kugonganisha macho na yule mdada mithili ya paka lilikua ni kosa kubwa!!! Walinyong'onyea na kupoteza nguvu,wakadondoka chini kama mizigo tii!!! Lile Jibaba likasogea karibu yao huku likitengenezea vitanzi tayari kwa ajili ya kuwanyonga,macho ya yule mdada yalishalainisha zoezi kwa kudhoofisha ile dawa waliyopakwa hivyo kuruhusu zoezi la unyongaji kuchukua nafasi kama kawaida!!!!
JE ITAKUAJE? MUUNGANIKO WA WANAKIJIJI UTAUKABILI MUUNGANIKO WA JESHI?
Usikose IJAYO

=NYAYO ZA KUZIMU--25.
(muda usiosogea)
=Young Chriss
Matumbo yalichemka,jasho liliteremka!! Wengine walizirai kwa uoga,na wengine walitamani kujimaliza!!
Vilio vya wamama na watoto vilimeza ukimya wote wa usiku,ile sehemu haikukalika kabisa! Wake waliwakimbilia waume zao ilihali na watoto vilevile!
Mzee Rama na mkewe waliumia sana kumpoteza wao mwana,japokua walikua saba lakini hawakuhitaji kumpoteza hata mmoja wao machoni pao,machozi vilio na mafua ya uoga na uchungu vilitawala,kila mtu akawa anatizamatizama nyuma kwa hofu ya usalama wake binafsi.
Wakati taharuki bado imeshika nafasi,miili ya watu waliobebwa koroboi zilipozima ilionekana tena ikining'inia kwenye ule ule mti wa muembe aliotundikwa mama Matata!! Mavazi yao waliyokua wamevaa hayakuonekana wala kujulikana yalielekea wapi,walikua wamevishwa majoho mekundu kama alilovishwa mama Matata na yote yakiwa na ujumbe ule ule uliosomeka BADO KIDOGO!! Masikio yao na midomo ilikua inavuja damu na huku macho na ulimi vikiwa vimetoka nje!! Walitisha sana,hasa wakionekana wakibembea na kamba zao nyekundu shingoni! Idadi ya waliokufa na kamba kwa ile siku ikawa ni tano tayari.je mchezo utaendelea vilevile?? Na sasa ni yupi alie kwenye zamu?? Maswali hayo yalijaza vichwa vya wanakijiji.
Ilibidi kifanyike kitu sasa,kukaa tu pale kwa kutegemea ni salama ilikua si sahihi,mzee Rama na mwalimu Baraka walijitolea kwenda kwa mzee Patili kwa lengo la kumpa taarifa ili awasaidie kwa lolote kunusuru maisha yao yaliyo mikononi,waliwaaga wanakijiji huku wakiwaomba wawaombee wafike salama kwani safari iliyombele yao ni ya kutisha,hofu ilikuwemo mioyoni mwao lakini hakuna jinsi jambo lile ilibidi litendeke,mke wa mzee Rama na wanae sita waliobaki walikua hawana matumaini kama baba yao atarudi,walimuangalia kwa huzuni huku wakimpungia mkono wa kheri,mwalimu Baraka nae alikua anajilaumu nafsini kwanini alikubali kuja kufundisha kijiji kile,ndio serikali ilimpangia lakini aliona alifanya kosa kuja lile eneo,ni bora angekataa hata kama ingehatarisha kibarua chake,mambo yanayojiri yataka moyo.
Safari ilianza,taratibu mwalimu Baraka na mzee Rama wenye baraka za usalama kutoka kwa wanakijiji walikua wanajongea,hofu waliyonayo mioyoni iliwafanya washindwe kujizuia kugeukageuka nyuma na mioyo kwenda mbio,lakini nyuso zao zilificha hayo,kila mmoja alikua anataka kudhihirisha kwa mzenzie kwamba haogopi.
Wakiwa kwenye mwendo mwalimu Baraka aliitoa simu yake iliyofeli mtandao tokea majuzi kwa lengo la kujua wakti,alishtushwa sana na alichokiona,muda uliokua unaonyeshwa na simu yake haukumwingia kabisa akilini! Ni muda mrefu umepita tangu giza liingie lakini bado saa ilikua inasema ni saa MOJA NA NUSU USIKU!! lile jambo lilimfanya mwalimu Baraka ahisi saa yake imepoteza majira lakini bado alipata maswali kichwani kwamba hii tabia ya kupoteza majira imeanza lini kwani alikua ameiseti saa yake hivyo hata likitokea jambo lolote bado majira huwa palepale,alipata hofu lakini hakutaka kumshirikisha mzee Rama,alinyamaza na safari ikaendelea,lakini ukweli ni kwamba muda ulikua hausogei,yani ulisimama palepale!
* * *
Julina baada ya kupewa somo zito na wenzake,aliituliza hofu yake,akatambua thamani ya mwanae na hakuwahi tarajia kwamba angekua mtu wa kumzaa mtoto ambaye angehitajika kwa ule muda,alijivunia hilo.Mzee Otongo hakutaka kumficha Julina,bayana alimjuza ya kuwa asipoteze muda kumsubiria mumewe kwani ni dhahiri atakua ameuwawa na Jeshi la 666 tangu yeye ni baba wa kiumbe hatarishi kwao,hii habari ilimsikitisha sana Julina japokua nae alikua na hisia hizo hizo japo hakua na uhakika,chozi lilimdondoka,alimpenda sana mumewe Kitanzi na hata ndoa yao haikufikisha hata miaka miwili,bado alikua na hamu nae na ukizingatia hajamuona mtoto ambaye mkewe alimleta ulimwenguni,ilitia huruma.
Kila mtu alie mule ndani aliuona usiku ni mrefu,walitamani kuona mwanga wa jua ukipendezesha tena macho yao,waliona usiku ni hatari kwao hivyo mioyo yao ilishikwa na tamaa kubwa ya kuona tena miale ya jua itakayoamsha matumaini yao,sauti za wadudu ziendeleazo huko nje zilizidi kuwaogopesha,hasa Julina.
Ngo! Ngo! Ngo! Sauti toka mlangoni iliwasili masikioni na kuwashtua kidogo,kama kawaida mama Halima alikimbilia dirishani na kuchungulia ni wakina nani,kisha akawatonya wenzie "ni wakina Madhifa!"
"wafungulie!"
mzee Patili akasema,
wakina Madhifa waliingia ndani kwa haraka huku wakihema kwa nguvu hali iliyowatisha na macho yao yalikua yanamimina machozi,kwikwi ikiwabana na kuwazuia kusema walilodhamiria,ilibidi mzee Patili awatulize kwanza ili waweze shusha presha na kusema kilichowaleta,baada ya kutulia wakasema
"Mama Linda na mumewe wamenyongwa!!"
kauli hiyo iliwafanya wakina mzee Patili mioyo ipasuke kwa mshangazo na kuanza kwenda kasi!!! Ilikua ni kama tamthilia kwenye masikio ya mzee patili aliewaona hao watu muda si mrefu,wakiwa kwenye taharuki na butwaa wakasikia hodi tena!! Ya Mara hii ilikua ni ya wakina mzee Rama na mwenzie mwalimu Baraka! Je itakuaje?
USIKOSE

NYAYO ZA KUZIMU--26.
(MUDA USIOSOGEA)
-Young Chriss
Nao pia wakasema kilichowaleta,watu watatu ambao ni mama matata,mtoto wa mzee Rama na mmama mmoja wa makamo wamenyongwa katika mazingira ya kutatanisha na aliewanyonga hajulikani,kwa ujumla taarifa za vifo zilizomfikia mzee Patili zilikua tano!! Alishangazwa na hiyo idadi,na si tu yeye hata wakina mzee Otongo na wakina Julina!! Hofu ziliwashika mpaka kwenye ukucha,puh! Julina akadondoka na kupoteza fahamu!! Mtoto aliekua amembeba aliwahiwa haraka na mama Halima na ilikua rahisi kwake kwa kua walikaa karibu,shughuli za kumpepea kumrudisha kwenye fahamu zikaanza haraka!! Mzee Rama na mwalimu Baraka wakapata kibarua cha muda cha kupepea huku wakina Madhifa wakiwa tu pembeni wakishuhudia hayo,uadui bado uliwatenganisha.
Baada ya kamuda kadogo Julina alirudi kwenye fahamu zake.
Uhasama uliokuwepo baina ya makundi mawili yaliyokuwepo pale ulionekana dhahiri,wakina Madhifa walijitenga kabisa na wakina mzee Rama kwani ndio wanahousika na uchomaji wa nyumba zao,vilevile mzee Rama hakujumuika nao kwa kudhani ku yote yajiriyo chanzo ni wao na alikua anawatizama wakina mzee Otongo kwa jicho baya kutokana na imani yao kua wale wageni pia huchangia kutokea kwa hali husika,mwalimu Baraka yeye hakua upande wowote kwani yeye si mwenyeji pale kijijini,mzee Patili aligundua huo mkanganyiko,kazi ya kuwatuliza wale watu wenye imani tofauti ziendeshazo mioyo yao ilibidi ifanyike,aliamini ya kua umoja utakaokuwepo baina yao ndio utakaokua silaha kubwa ya kujilinda na kukabiliana na linalowasibu,elimu hasa juu ya kinachoendelea ilihitajika kwenye vichwa vyao na vya wanakijiji wote ili iwe kama chachu ya mabadiliko na mwanzo wa mapambano,alitumia busara,aliwauliza wakina mzee Otongo kama wanaweza jongea wakajibu watajitahidi,akawapa ujumbe wakina Madhifa ya kwamba wakawaite wenzao yani jamii ya wawindaji na wakutane kwa mama Kurwa,walitii walichoambiwa,wakatokomea kwenda kuwasilisha,kisha akawaambia wakina Julina na wakina mzee Otongo wainuke na safari ianze ya kuelekea huko walipotokea wakina mwalimu Baraka,yani kwa mama Kurwa ambapo ndipo wanakijiji walipokusanyika,akachukua vibuyu vyake viwili kisha safari taratibu ikaanza wakiwemo watu nane;mama Kadogo na mzee Otongo waliokua wanachechemea,Julina na mama Halima aliembeba mtoto,mzee Patili mwalimu Baraka na mzee Rama.Japokua walikua wengi lakini bado kale kamchezo ka kuangaliangalia nyuma hakakukoma,kila kaupepo kalipopiga miili yao iliiteka misimko ya kioga hasa Julina alieng'ang'ania awe katikati ya watu,ni sauti za miguu yao tu ndio ilyosikika walipokua wanapita,kote kulikua kimya ukiondoa vikelele vidogodogo vya vijidudu vya usiku,muda huo wote waliokua njiani mzee mzee Patili alikua anafanya kazi ya kuvitikisa vile vibuyu vilivyomkononi,haikujulikana kazi yake ni nini na hakuna mtu aliemuuliza,walimuacha afanye mambo yake kwa uhuru.
Hatimaye walifika walipokua wanaelekea,watu waliokua wamejikunyata kwa kukosa matumaini waliamka na kumlaki mzee Patili,aliwapa mwanga wa kufanikiwa,akikua mwema kwao kwa ule muda,walisahau kabisa walichokifanya huko nyuma,ila ujio wa wakina mama Kadogo na mzee Otongo uliwashtua wanakijiji,moja kwa moja minong'ono ikaanza kururuma....mzee Patili hakuvumilia hilo,aliufungua mdomo wake kwa ukali akasema
"acheni upumbavu wenu usio na msingi!! Huo ujinga ndio upelekeao hali kua mbaya zaidi na hautupi unafuu wowote! Nani asiemjua huyu mzee Otongo?? Si nawauliza nyie! Ni mara ngapi alikua anakuja hapa kijijini na kuwasaidia matatizo mbalimbali?? Iweje leo unaufungua mdomo wako na kumnyooshea kidole,mshausahau wema wote alioutenda kwenu? Mbona mnakua na vichwa vya panzi na mioyo y kutu!"
wanakijiji wote walitulia na kusikiliza kwa makini na roho zao zilianza kuwasuta,mzee Zptili akaendelea kunena..."umoja wetu ndio unaohitajika,kugawanyika kwetu ndiko kunapoipa mwanya kushindwa kwetu,nawaambia kama tusipokua pamoja,shingo zote zilizokuwepo hapa zitaonja kamba nyekundu kama waliopita!! Tutanyongwa kama kuku!!"
alizidi kusisitiza kwa sura ya mkazo,muda si muda wakina Madhifa wakaingizana,ukimya bado ukawa umetawala,masikio na macho yao alipewa mzee Patili aliesimama mbele.Baada ya mzee Patili kurudufisha imani za waliokua wanamsikiliza,aliwakaribisha wakina mzee Otongo na mama Kadogo kwa lengo la kutoa somo juu ya hali iliyojiri,waliwadadavulia na kuwanyumbulia wanakijiji kwa undani tangu walipotokea na nini kimewaleta hasa.
JE HUU MUUNGANO UTAWASAIDIA MBELE YA JESHI LA 666?? USIKOSE!!

-NYAYO ZA KUZIMU--28.
(muda usiosogea)
-MTUNZI;Young Chriss
Lile jitu baada ya kuwafunga vitanzi wakina Mrisho alianza kuwaburuza kama nyama!! Halikujali kitu chochote juu yao na wala sura yake haikuonyesha hata chembe ya kulifikiria hilo.Walipowadia kwenye mti mmoja wa mkuyu,waliwatundika wale watu,wakaungana na shingo zingine zilizoonja kamba nyekundu, utofauti wao na wale waliotangulia ni kwamba wao walinyongwa bila mioyo yao iliyochukuliwa na yule mdada mithili ya Paka aliekua na mahitaji nayo,walibaki na mashimo tu yaliyokua yanamimina damu!!!
Ile Mioyo iliingizwa kinywani mwa yule dada na moja kwa moja ilianza kutafunwa mithili ya keki huku lile jibaba likishuhudia,baada ya kumaliza lile tendo ghafla walibadilika na kuchukua sura za waliowauwa!! Lile jibaba liligeuka na kua Tabwe huku yule mdada akiichukua sura ya Mrisho!! Taratibu huku wakiwa wameshikilia mifuko isiyojulikana ilitokea wapi walianza safari ya kuelekea kule wanakijiji walipo!! Hapakukalika tena!! Hatari ilizidi kuchukua nafasi!!
* * * * * * *
Baada ya muda mrefu kupita bila ujio wa wakina Mrisho mzee Patili na wanakijiji wengine walianza kupata hofu,akili zao zilianza kuruhusu mawazo mabaya kupenya na mioyo yao ilianza kupokea taarifa za simanzi,wanakijiji waliokua hawajapakwa dawa walikua na hofu mara mbili kwani wao walijiona si salama ulikilinganisha na wenzao,walitamani wakina Mrisho waje haraka ili nao miili ipate kunawiriwa na dawa ambayo waliiamini kwa asilimia zote itakua kinga madhubuti kwao dhidi ya hali endelevu,walisali mioyoni,waliomba sana mungu wao apate kutanakabali sala zao.
Muda si muda Mrisho na Tabwe feki waliingia,wanakijiji waliokwisha kata tamaa walilipuka kwa furaha na kuwalaki kwa upendo ulioonyesha matumani,masikini ya mungu hawakufahamu kwamba wale siyo,mzee Patili aliupokea mfuko aliopewa na haraka akawaambia wale waliokua bado hawajapakwa wajipange mstari,wakapanga,akaanza kuwapakaa kama ilivyokua mwanzoni ila sasa hivi alihusika kwenye kuwapaka wote yani wanaume na wanawake wakiwa wamepanga mstari mmoja tu,kutoka na dawa waliyopakwa wanakijiji wengine Tabwe na Mrisho walishindwa kustahimili,walisogea pembeni mbali na wanakijiji wengine,kujitenga kwao kulimpa kidogo maswali mwalimu Baraka alieamua kuwafuata kwa lengo la kuwapongeza kwa ujasiri wao,alipowakaribia aliwapa mkono wa kheri uliopokelewa na Mrisho ambaye ni yule mdada mwenye roho ya paka,kha!! Alishtuka mno mwalimu Baraka!! Mkono wa Mrisho ulikua wa baridi mno mithili ya barafu,hali hiyo ilimpelekea autoe mkono wake haraka na kuuliza...
"we Mrisho mbona mkono wako wa baridi hivi???"
"kawaida tu,si unajua tulikua tunakimbia ili tuwahi!!"
alijibu Mrisho,mwalimu Baraka hakuridhika na lile jibu hivyo akauliza tena
"sasa kama mlikua mnakimbia mbona mlichelewa??"
swali hilo lilifanya kidogo Mrisho akwame,alimuangalia mwenzie Tabwe aliewahi akajibu,
"tatizo kule kwa yule mzee ndo' kulituchelewesha,madawa yaliku mengi mno!!"
"ah-ahaa! Ila poa haina tatizo,hongereni bwana kwa ujasiri wenu mliouonyesha! Bella alikua ana wasiwasi kweli..teh! Teh!"
mwalimu Baraka alimtania Tabwe kuhusu mchumba wake Bella,cha ajabu uso wa Tabwe ulimdhihirishia mwalimu Baraka ya kua halikua hajui kiongeleachwo,
"Bella?? Ndio nani??"
aliuliza Tabwe swali lililozidi kumshangaza mwalimu Baraka!!
Moyo wa mwalimu ulisita,alipata hofu,hakutaka kukaa tena pale,taratibu aliaga na akajiondoa lile huku maswali kichwani yakizidi kupapaliwa na kuchipukia.
Lile jibaba lilimuangalia mwenzie alie ndani ya sura ya Mrisho kisha akamuuliza..
"unadhani atakua amegundua chochote??"
"sidhani,ila kama ukiniuliza ni moyo wa nani ninaoutaka kwa sasa,dhahiri nitakujibu ni wake!"
"ile dawa waliyopakwa nayo itaanza kufanya kazi muda gani? Mbona kama inachelewa??"
"tuliza munkari,ipe kama nusu saa,utaona majibu yake nadhani unafahamu huwa sibahatishi"
alijigamba bimdada,
"nafahamu hilo,ila ile dawa waliyoipakaa ni kali mno! Nadhani uliona jinsi tulivyokua tunapata shida alipokuwepo yule mbaba"
"ni kweli,ila siwezi kuondoka mpaka nione ikifanya kazi!"
"sawa."
maongezi yakakomea hapo.
Hayawi hayawi yakawa!! Dawa waliopakwa watu wa awamu ya pili ilianza kufanya kazi bara-bara!! Miili yao ilianza kuwasha hatari!! Na kila walipojikuna ngozi ilitoka na kuruhusu damu iruke kama bomba!! Makelele ya kuomba msaada yaliteka ile sehemu!! Muwasho wa ajabu usiovumilika uliwafanya wawe machizi kwa kuranda huku na kule wakipiga makelele kwa nguvu!!!! Mzee Patili alishikwa na butwaa!! Wanakijiji walitawaliwa na taharuki!! Walipotizama wakina Mrisho wako wapi,HAWAKUWAONA!! Mungu wangu!! Wale waliokua wanawashwa wakaanza kukauka na kuwa magofu meupe kama chumvi!!
JE NINI KITAENDELEA? Usikose sehemu IJAYO.

-NYAYO ZA KUZIMU--29.
(muda usiosogea)
-MTUNZI;Young Chriss
Wale waliokua wanawashwa wakaanza kukauka na kua magofu meupe kama chumvi!!!
Kilio kilichobeba uchungu na uoga kilipata kutoka vizuri toka kwenye midomo ya wakina mama na watoto,vilevile mioyo ya wakinababa ilikita kwa nguvu na macho yao yalitoka kwa kutoamini,ulikua ni kama mchezo wa kuigiza,sehemu ile yote ilitawaliwa na magofu ishirini na mawili yote yakitokana na ile dawa ya awamu ya pili! Wanakijiji walipungua kwa kiasi kikubwa,watoto wengi walipoteza wazazi,wanawake wengi walipoteza waume zao,na hata vile watu wengi walipoteza watu wao wa karibu,simanzi iliyoje!!!
Mzee Patili alichanganyikiwa kabisa,hakujua cha kufanya japokua mzee Otongo alikua anajitahidi mno kumtuliza,alijiona yeye ndie muuaji na hata baadhi ya wanakijiji walianza kufikiria hivyo,walifikiria ya kwamba vile vifo ni dhahiri vimesababishwa na mzee Patili ilihali wengi wao bado walikua kwenye tahamaki ya njia panda hasa baada ya wale walioleta dawa kupotea kiajabu machoni mwao!!
Mama Kadogo aliutumia ule mwanya kuita rai na kuteka hamsha za wanakijiji,kwa kujiamini alisimama mbele yao na kusema
"Jamani..jamani!! Naomba tusikilizane! (ukimya ukatawala lakini bado vikwikwi na vimafua vya vilio vilikua vinachukua nafasi)....katika vita hii tunayopambana nayo kufa kwa mtu au watu isiwe kitu cha kutushangaza,mtu yeyote kwa muda wowote anaweza akafa kwenye mapambano haya hilo inabidi liwe kichwani,naomba tusiruhusu roho za simanzi ziweke kiza kwenye njia yetu bali roho ya ushupavu na ya kusonga mbele,ni hakika tumezidiwa akili na hili jeshi la 666 katika huu mchezo,waliutumia ipasavyo ule mwanya tuliowapa wa kuwatuma wale vijana,nadhani hilo halina maswali...tumeona kwa macho yetu walivyopotea kiajabu na kuudhihirishia uma ya kwamba wao sio wale tuliowategemea!"
haraka Mwalimu Baraka alidakia
"hakika mama,hakika!! Wale hawakua wakina Mrisho kama tulivyodhani,mie mwenyewe naweza nikasema hivyo kwa ushahidi wangu mdogo nilioushuhudia,walikua ni watu wa baridi mno! Na hata baadhi ya maswali niliyowauliza walishindwa kabisa kujibu,kusema ukweli nilipata hofu lakini sikuwa na uhakika asilimia mia hivyo nikaamua nijitoe lile eneo kimyakimya!"
maneno hayo ya mwalimu Baraka yaliamsha minong'ono miongoni mwa watu,mama Kadogo aliwatuliza na kisha akaendelea kunena..
"ni matumaini yangu dawa tulizopaka zina msaada kwetu,bado ninaamini hivyo japokua hili tukio la wakina Mrisho linaweza kuwatia mashaka mioyoni,hapo ndipo tunapoweza kurudia kauli yangu ya mwanzoni ya kwamba walituzidi akili,nahisi kuna kitu walichokifanya hawa jeshi ambacho bado hatujakifumbua...."
(kabla hajamalizia mzee Rama kwa jazba alidakia)
"sasa tufanye nini?? Hamuoni ya kwamba tunaendelea tu kufa!! Au nyie bado hamjatosheka???"
kauli ya mzee Rama ilizua tena minong'ono na malumbano,baadhi ya wanakijiji walionekana kumuunga mkono na baadhi yao walionekana kumpinga,makundi mawili yakazaliwa miongoni mwao!! Ni dhahiri imani zao haba zilianza kuwachonyota,mzee Patili taratibu alisimama na kuelekea pale alipo mama Kadogo kisha akawaomba utulivu kwa muda ili apate kunena,wale waliokua bado na imani nae walifunga midomo yao na kumpa masikio lakini wale ambao imani zao zilitiwa doa hawakujali hilo,waliendelea kururuma tu,mzee Patili akatoa tamko..
"kama imani yako haiko nami tena,sitofanya jitihada zozote kuiinua maana umeamua hivyo,kama nilikua nanyi tokea ujana nikiwahudumia na bado imani zenu zina madoa kuhusu mimi,hakuna chochote ninachoweza fanya kwenu kwa sasa.Ninaelekea upande wa kulia nilipotokea,kama bado una imani nami waweza nifuata,kama huna imani nami waweza kubaki.."
sura ya mzee Patili ilionekana si yenye furaha,alikua anawaza jambo na dhahiri alionekana ameumia,alishika njia ya kuelekea nyumbani kwake na kundi la watu huku nyuma lilimfuata akiwemo Julina mwenye mtoto aliebeba matumaini yao,bila hata kuonyesha aibu usoni mzee Rama nae na wenzake walioonyesha kutia shaka juu ya mzee Patili nao walikuwemo ndani ya msafara wakiivuta miguu yao kumfuata,hawakufanya hivyo kwa kupenda bali iliwabidi kwani mtoto ambaye ndie ngao ya matumaini alikua upande ule hivyo hawakua na jinsi,mzee Rama bado alikua na gubu jeusi lililokua linamkereketa,hakupendezewa kabisa na ile hali ya uongozi wa mzee patili,wivu ulimkua unamsumbua kwa kiasi kikubwa,alitaka yeye ndie awe anasikilizwa na yeye ndie awe anatoa amri,wivu ulimshika mishipa yake ya damu,akili yake ilimtuma amuibe yule mtoto wa Julina,alifahamu fika ya kua akimmiliki yule mtoto jamii nzima itamsikiliza yeye kwani ndie atakaekua ameshikilia matumaini yote ya wanakijiji,atafanyaje sasa?? Alijiuliza kichwani mwake,baada ya kupata jibu haraka alimvuta mwenzie pembeni na kumwambia..
"unataka kufa na wewe,ama??"
swali hilo lilimshangaza alieulizwa,kiuoga nae akajibu..
"hapana!!"
"sasa nisikilize nitakayokuambia..."
JE ANATAKA KUMUAMBIA NINI?
UADUI WA MZEE RAMA MWISHO WAKE NI NINI??
Usikose sehemu ijayo.

-NYAYO ZA KUZIMU--30.
(muda usiosogea)
-MTUNZI;Young Chriss
"unataka kufa na wewe ama??"
swali hilo lilimshangaza alieulizwa,kiuoga nae akajibu
"hapana!"
"sasa nisikilize nitakayokuambia.."
"enhe.."
"najua wewe ni mwenzangu na ninakuamini hautoniangusha,hivi we unadhani haya yote yanayojiri ni sababu ya nani??"
"mh...kusema ukweli mie sijui!"
"we unahisi ni nani??"
"mmmh....labda ni hawa wageni au...."
"ah-ah! Hawa wageni waliruhusiwa na nani??"
".......mzee Patili!"
"unavyodhani ni nani sasa hivi anatuua??"
"si lile jeshi la 666 walilotuambia!!"
"..kwani wale ndio waliowapakaa nyie dawa??"
"hapana! Ni mzee Patili!"
"majibu yote yapo wazi kama unavyoona,huyu mzee ndio kikwazo kwetu,na hivi ninavyokuambia ni kwamba lengo lake si kukabili jeshi la 666 kama anavyotudanganya bali anataka amtumie yule mtoto kwa malengo yake binafsi,yani kujinyanyua na kufanikisha hamu yake ya uongozi!! Hivyo basi ili atudhoofishe na asafishe njia yake anatupunguza idadi kama unavyoona...!!"
haikuishia hapo tu,kukaa kwake nyuma ya ule msafara alikutumia kama ngazi ya kuigeuza mioyo ya wanakijiji,alipenyeza uongo kwa walio karibu na kufanikiwa kuiteka mioyo yao yenye imani haba,na alitamani zaidi.
Baada ya muda msafara wa wanakijiji uliwasili kwa mzee Patili,walishangazwa na hali waliyoikuta ikiwemo mzee Patili mwenyewe,mlango haukuwepo sehemu yake na mwanga wa mwezi uliokuwepo uliruhusu kuonekana unga fulani wa manjano chini mzee Patili aliougundua kwamba ni dawa ile aliyoiagiza,alama za miburuzo zilizokuwepo chini ziliwatia mashaka hivyo wakasogeza koroboi na kuanza kuzifuatilia mpaka pale zilipowafikisha kwenye miili ya wakina Mrisho iliyokua imetundikwa!
Macho yaliwatoka kwa kushuhudia zile maiti zilizokua zinaning'inia na mashimo vifuani,machozi na simanzi havikuzuilika kuwa miongoni mwao,miili ile ilishushwa na kumpa ruhusa mzee Patili kuikagua kisha akatoa neno..
"watu waliotumwa ni wazi walivamiwa! Nadhani mazingira husika yanaeleza hivyo,dawa niliyoiagiza tumekuta imemwagika,mlango umevunjwa,vilevile wamenyongwa! Hiki ni kielelezo tosha ya kua dawa iliyoletwa kule haikua sahihi.."
alivuta pumzi kidogo kisha akaendelea
"miili ya wakina Mrisho japokua imenyongwa kama ile mingine lakini kuna utofauti juu yao,utofauti huu unatudhihirishia ya kwamba kuna kiumbe kingine ambacho ni hatari kwetu kimeongezeka,na ndio hasa kinachohusika na hii mioyo iliyobebwa! Inatubidi tuongeze kinga yetu!"
mzee Patili akanyamaza kidogo,ila taratibu mzee Otongo alimkaribia na kuanza kumnong'oneza kitu hali iliyohamsha vimaongezi vya chinichini hasa kutoka kwa mzee Rama aliekua anapigilia misumari maelezo yake ya uongo aliyoyaingiza ndani ya vichwa vya watu huku akihakikisha mzee Patili hagundui hilo.
Baada ya mzee Patili na Otongo kujadili waligundua cha kufanya japokua ilikua vigumu kuwaeleza watu,kazi ngumu ilibidi ifanyike na pia ilihitaji watu jasiri watakaojitolea kuifanikisha,baada ya kujiulizauliza sana mzee Patili aliamua apasue jipu,
"tunahitaji dawa kwa ajili ya kuongeza kinga yetu madhubuti,kama nilivyowaambia hapo kabla ya kwamba ni lazima kinga yetu iendane na mazingira husika,sijamaanisha ya kuwa tuliyonayo haifai,hapana,ila inabidi tuiongeze nguvu..."
alishindwa kuendelea,mzee Otongo ikabidi aendeleze alipoishia..
"tunahitaji Mdigidigi!!"
"Mdigidigi!!!"
wanakijiji walihamaki,
"ndio Mdigidigi!!...na kama tunavyojua haipatikani hapa karibu......."
"ndio! Ni mpaka mtoni!!"
"haswaa!..Mpaka mtoni!...inabidi tuwe na ule mti ili tuweze tengeneza dawa,tatizo ni kwamba tutaipataje?"
Otongo aliuliza,
mama Kurwa akatoa maoni yake
"inabidi watu wafuate kama ni hivyo!!"
kauli hiyo ilizua mjadala mzito,hakuna mtu alieonekana yu tayari kufanya hicho kitu kwani waliona ni kama kujiingiza kwenye mdomo wa kifo wenyewe,kila mtu alitaka kuilinda roho yake.
Katika hali ya kushangaza mzee Patili alinyamazisha watu na kuwataarifu ya kwamba ataenda yeye mwenyewe,taarifa hiyo badala ya kunyamazisha mjadala iliuzua zaidi,uamuzi wa mzee Patili kwenda kutafuta ule mti ilipokelewa na mawazo tofauti,asilimia nyingi ya watu walionekana kutoafikiana nalo huku wengine wakiliunga mkono....wakati taharuki bado ikichukua nafasi sauti ya mzee Rama tokea nyuma kabisa ilipata kusikika ikisema..
"mimi nitaenda huko mtoni!...mimi nimejitolea kwenda!! Nitumeni!"
hakuna mtu alietegemea kuisikia hiyo kauli tena toka kwenye kinywa cha mzee Rama,miguno na maswali ya chinichini ilizuka lakini hivyo vyote havikubadilisha uamuzi wake,alijisogeza mbele kabisa ya umati huku akimtizama mzee Patili,kisha akarudia kauli yake..
"nitume mimi!!"
Je KiPI KIMO KICHWANI MWA MZEE RAMA? Kwanini anataka kazi wengne wanayoiogopa?
USIKOSE SEHEMU IJAYO!

NYAYO ZA KUZIMU--31
(mwanga wa giza)
lile jibaba nalo likaanza kutapatapa kama samaki nchi kavu!! Macho ya wanakijiji waliokua wemejificha hayakuamini yalichokishuhudia,lile Jibaba ilikua kama mtoto kwa jinsi lilivyokua linajibaraguza na kurukaruka huku na kule kwa mitindo yote,ni dhahiri miale ya jua lililochomoza ilimuunguza kupita kiasi na alishindwa kabisa kuvumilia hilo,alitia huruma mno kwa jinsi alivyokua akilalamika,waweza sahau mabaya yote aliyoyatenda kwa jinsi alivyokua anateseka,hatimaye mwili wake ulikua majivu kabisa na wa yule mdada pia,hakuna kilichobaki juu yao na huo ndio ukawa mwisho wao,chereko nderemo na vifijo zilitawala.
Je wanakijiji wataishi kwa amani sasa?? Ni swali lililohitaji ufumbuzi mzito.
* * * * * *
(Dar es salaam,Msasani)
mchungaji Josiah alikua amejipumzisha juu ya kitanda chake sita kwa sita akiitawanya miguu na mikono kwenye pande zote nne za kitanda,ni dhahiri huduma ya kiroho aliyoifanya jana usiku ilimchosha mno kwani japokua jua lilikua lishachomoza mwili wake bado ulionekana kutamani kitanda ambacho hakikushushiwa hata neti ya kumzuia na mbu,alijigeuza kivivu na kuendelea kuvuta makasia ya usingizi mpaka pale aliposhtushwa na mlio mkali wa simu yake ya kichina yenye muito wa nyimbo fulani ya injili ya muimbaji maarufu nchini,macho yake yaliyotawaliwa na mang'amung'amu ya usingizi yalifunguka kwa mbali kuangalia ni nani anaepiga,alishtushwa kuona ni Askofu Emmanuel haraka aliiweka simu sikioni..
"shalom Askofu!"
"shalom Josiah...vipi unaendeleaje?"
"safi tu namshukuru mungu aisee.."
"ni kweli mungu aliejuu ashukuriwe,sasa Josiah..."
"naam Mtumishi!"
"embu fika hapa kanisani mara moja kuna kitu cha muhimu inabidi tujadiliane"
"haina shida mtumishi wa mungu,nitakuwepo hapo muda si mrefu!"
"sawa,bwana mungu awe nawe.."
"amina,awe nawe pia mtumishi.."
maongezi yakakata,mchungaji Josiah aliekua amechoka kama mbwa kutokana na shughuli pevu aliyofanya jana aliamka kwa kujivutavuta na kuelekea bafuni kupata maji,hakuweza kabisa kumbishia Askofu hivyo hakua na jinsi zaidi ya kutekeleza kile alichoambiwa na mkubwa wake ukizingatia yeye bado ni mchungaji mwanafunzi kwani si muda mrefu tangu aanze rasmi shughuli zile za uchungaji.Ilichukua kama dakika thelathini na tano kwa mchungaji Josiah kumaliza kabisa zoezi la kujiandaa,alipanda daladala chapchap na kufika kanisani haraka tu kutokana na ukaribu uliokuwepo,alipoingia tu kanisani macho yake yaliweza kumuona Askofu Emmanuel akiteta jambo na mtu fulani alievalia suti nyeusi,kabla hata ya yeye kufika walishamaliza maongezi yao na yule mtu akapanda gari na kuondoka,Askofu Emmanuel alimkaribisha mchungaji Josiah na moja kwa moja walielekea ofisini walipowakuta watu kama kumi wenye vialama vyeupe shingoni vilivyoashiria ya kwamba ni wachungaji,baada ya salamu za hapa na pale majadiliano yalianza baada ya kufunguliwa na sala nzito toka kwa Askofu,kikao kile hasa kilikua kinahusu usambazwaji na uenezaji wa neno la bwana kama ilivyoagizwa,kilikua ni mahususi kwa ajili ya kujadili mikakati itakayowezesha injili kufika mahali ambapo hapajafikika,kanisa lilihitaji kufungua matawi yake zaidi ili iweze kuwafikia watu wengi zaidi waliohitaji huduma za kiroho sehemu mbalimbali za nchi hasa vijijini,baada ya masaa mawili kikao kilikwisha kwa kumteua mchungaji Josiah asimamie shughuli ya kwenda kusambaza injili mkoani mbeya na kutia msingi wa kanisa,hakuamini kilichotokea kwani aliona ile ni kazi kubwa ambayo hakustahili apewe,haikua na jinsi,Askofu Emmanuel alimuamini na ukizingatia mchungaji mzoefu Isaya alikuwepo mkoani Arusha kiroho,ilipangwa siku ya kufunga safari na idadi ya watu watakaokuwepo kisha mchungaji Josiah alirudi nyumbani kwake kwa ajili ya kuendelea na mapumziko.
Alipojirusha kitandani usingizi haukuja kama alivyotegemea,moja kwa moja akili yake ilianza kupitia kile alichoambiwa na kidogo kupata mawazo,ila katikati ya yale mawazo taratibu tabasamu lilichomoza usoni mwake na kuupendezesha uso wake mrefu wenye dimpoz,hakuna mwingine alieleta hilo tabasamu zaidi ya Rachel Mwakatwila mwanakwaya mahiri pale kanisani aliyewekwa kwenye orodha ya wale waendao kutoa huduma,moyo ulilifurahia hilo,fursa adimu aliyokua anaisaka imekuja mikonomi mwake,nini nataka zaidi?? Kazi ni kwangu!! Alijiambia mchungaji Josiah.
* *
Jumatano alfajiri na mapema mchungaji Josiah,Rachel na watumishi wengine wawili walianza safari ya kuelekea mkoani mbeya kwa kutumia bus,kitendo cha mchungaji Josiah kupewa fursa ya kukata tiketi ilitumika vema kwani aliutumia ule mwanya kukata tiketi iliyomueka karibu na Rachel kitulizo chake cha moyo,safari nzima ilitawaliwa na vijistori vya hapa na pale na vicheko vya haja,Josiah alisahau kabisa cheo chake cha uchungaji mbele ya Rachel,stori zilinoga,ila mwishowe Rachel alibebwa na uchovu wa safari akamlalia mchungaji Josiah begani.
* * * * *
USIKOSE SEHEMU IJAYO UPATE JUA KILICHOJIRI.
Like zaidi ya tatu zahtajika ili simulizi isonge.ONE LOVE.

NYAYO ZA KUZIMU--32
(mwanga wa giza)
ILE YA JANA NI SEHEMU YA 31 HII YA LEO NI SEHEMU YA 32 SAMAHANI SANA KWA KUWA CHANGANYA WATU WANGU WA NGUVU
kila mara Josiah alipomtizama Rachel alielalia begani kwake alijihisi amani,alitamani alalie na kwenye moyo wake vilevile,hakujua cha kufanya ili aweze muingiza Rachel kwenye system ukizingatia cheo chake cha uchungaji,kuhisiwa vibaya mbele ya jamii na kunyooshewa kidole vilimtia hofu pia hisia za kukataliwa zilizidi kumtisha,alisema tu na moyo wake mkavu unaoumia.
Mwendo wa kasi wa bus ulifanya baadhi ya abiria walipuke kwa maneno wakimshutumu na kumsema dereva,makelele na malalamiko yao yalimuamsha mchungaji Josiah toka kwenye usingizi mzito wa mawazo juu ya Rachel aliokua nao,hakuchangia chochote kwani hakuna alichoshuhudia ila aliona watumishi wenzake wawili David na Rio wakijibizana na baadhi ya abiria juu ya mwendokasi wa gari,alipomtizama Rachel alikua bado amelala hivyo nae hakujua lolote linalojiri.
Baada ya muda kidogo bus lilipaki kwa ajili ya kuruhusu abiria wapate cha kutia tumboni,mchungaji Josiah alimuamsha Rachel aliekua bado amelala kisha wakaenda kupata msosi na kurudi ndani ya gari,muda si mrefu gari nalo lilijiondoa lile eneo na kuendelea na safari ya kuelekea jijini mbeya,shibe na uchovu vilimlemea mchungaji Josiah na sasa ikawa ni zamu yake kulala,usingizi mzito uliombeba ulimpeleka mpaka kwenye ardhi ya ndoto ya ajabu isiyopata kusemeka,alijiona yupo kwenye giza zito nene na hajui pa kuelekea,miguu yake iliyokanyaga chini ilihisi baridi kali na kufanya mwili wake uitike kwa mtetemeko,moshi mzito ulimzunguka na kumfanya akohoe huku akihangaika kuitafuta pumzi kwa hali na mali ilhali moyo na akili yake vikishika kasi ya uoga,alikohoa na kukohoa,alikohoa mno mpaka kifua kikaanza kuita kwa maumivu!! Alikohoa mpaka macho yakaanza kububujika machozi na kuhisi kichomi!! bado kikohozi hakikukoma hata kidogo,aliendelea kukohoa tena zaidi na zaidi mwishowe akaanza kukohoa damu!!! Mapigo ya moyo yalienda sawa na mbio za farasi wa mashindano,mzunguko wa kasi wa damu ulifanya baridi alilokua nalo lipotelee,joto liingie na kuruhusu vijasho kuchuruza mpaka sehemu za siri,kila alipojitahidi kuzuia kile kikohozi ule moshi ulizidi ongezeka na kumpalia hivyo kutompa machaguzi,mishipa ya uso ilimsimama na koo nalo likaanza kuuma!! Koh!-koh!-koh!-koh!-koh! Bado alizidi kukohoa!!....mchungaji Josiah alianza kushindwa kumudu mwili wake,mkojo ulianza kumchuruza na kufanya nguo yake ya ndani kuwa tepetepe,bado kikohozi hakikukoma wala kupungua kasi!! alitia huruma na imani mno kwa jinsi alivyokua anahangaika,alishindwa kabisa kusimama kwani miguu ilikwisha nguvu hivyo akapiga magoti na kuendelea na lile zoezi la kukohoa tena sasa akihisi mkono umemkaba shingo!!! alizidi kutoa damu na kutapatapa mpaka pale alipoisikia sauti nzito isiyojulikana imetokea wapi ikimwambia RUDI ULIPOTOKA!!!! kisha kufuatiwa na kicheko kikali cha kishetani!! Ha!-ha!-ha!-ha!-ha!-ha!-ha!
Baada ya hayo maneno mchungaji Josiah alishtuka toka kwenye usingizi huo mzito kwa pupa na kuwastua abiria wengine waliokuwepo karibu ikiwemo Rachel alie jirani.Rachel kwa tahamaki alimuuliza mchungaji...
"vipi mtumishi,kuna nini???"
mchungaji Josiah alishindwa kujibu,alionekana akihema kwa pupa huku akipepesapepesa macho kushoto na kulia kuhakikisha mazingira aliyopo,baada ya kutulia kidogo ndipo alipoanza kumuhadithia Rachel kile alichokiona kwenye ndoto,Rachel alishtushwa pia na zile habari na kumtaka mchungaji Josiah wasali ili mungu atie mkono katika safari yao,walishindwa kuwashirikisha watumishi wenzao kwani walikua usingizini,wakiwa katikati ya sala walisikia sauti kali za abiria kisha ukafuata mlio mkali Puh!!!! presha kali iliwasukumiza mpaka mbele na kujigonga kwa nguvu!! gari liligonga!!....muda si muda gari nalo likaanza kubiringita kwa nguvu!!! Vilio vya maumivu na uoga vilitawala ndani ya gari!! Baada ya dakika kama tano gari lilitulia huku bado vilio vya baadhi ya abiria vikiskika kwa nguvu vikiomba msaada,wengi wao walikua kimya huku miili yao ikivuja damu,wengine walionekana wakilia huku wakigusa sehemu waliyodhurika au kujeruhiwa,watoto wadogo wawili wenye miaka si juu ya mitano walionekana wakiwa wamelaliwa na gari hivyo sehemu kubwa ya miili yao ikawa imesagika,haikuhiaji utaalamu wowote,walikua wamekufa,hamaki mmama mmoja mjamzito alionekana tumbo limepasuka!! Ilitia huruma na ilisisimua kwa kutisha!! Damu iliyomwagika ilifanya nyasi zote zilizokuwepo kuwa nyekundu,lile eneo lilikua kama machinjioni!!
Huku akijikokota taratibu kutokana na maumivu mazito aliyokua anapata mchungaji Josiah alipata kuita kwa taabu.."Reeecho!!" hakuna aliyeitika,nae muda si muda alipoteza fahamu!!
*
JE NINI KITATOKEA??? .NAOMBA MAONI YAKO ILI NIKULETEE MFULULIZO MZIMA WA STORI HIZI....................................................ASANTE SANA

Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon