Halmashauri ya jiji la Mbeya ambayo ndio mmiliki wa timu ya Mbeya City football Club ilikutana na
bodi ya Michezo ya jiji inayosimamia uendeshaji wa timu leo tarehe 23.02.2015 kujadili muenendo
mzima wa mchezo wa timu yetu dhidi ya Young African uliochezwa tarehe 22.02.2015 pamoja na
matokeo yake
.
Katika kikao hicho,mmiliki pamoja na bodi yake walipitia taarifa na rejea ya mchezo husika na
kugundua mambo yafuatayo:
1. Kiufundi timu ilicheza vizuri na kwa kiwango cha hali ya juu ikilinganishwa na wapinzani wetu,
ila ilikosa kitu kimoja tu nacho ni ushindi.
2. Mchezaji David Abdallah Buruhani ambaye alikuwa golikipa katika mchezo huo alifanya
makosa binafsi na ya makusudi yaliyoigharimu timu kukosa ushindi katika mchezo husika.
Makosa ya mchezaji huyu katika mchezo huo yalikuwa yanafanana na baadhi ya makosa ambayo
alishawahi kuyafanya huko nyuma na kusahihishwa.
Baada ya kupitia rejea kadhaa ilibainika kuwa makosa mengi ya aina hii yamekuwa yakifanyika
katika baadhi ya mechi hasa zinazohusisha timu zenye ushawishi
Mazingira mazima ya makosa yote hayo yamezingirwa na mashaka makubwa
ambayo ni vigumu kujiweka mbali nayo akiwa kama mhusika mkuu.
Baada ya uchambuzi wa nyaraka mbalimbali na rejea zake, mmiliki ambaye pia muajiri wa
mchezaji husika amemsimamisha na kumuondoa kikosini mpaka hapo atakapomjulisha vinginevyo.
Halmashauri ya jiji la Mbeya imesikitishwa na mazingira mazima yaliyojitokeza ya kupoteza
mchezo huo.
Ni kweli mchezo wa mpira wa miguu ni mchezo wa makosa ila aina gani na mazingira yapi
ya kosa husika ni changamoto na kushinda na kushindwa ni sehemu ya mchezo ila umeshindwa je
na katika mazingira yapi ni changamoto kubwa zaidi.
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon