Dar es Salaam. Matumizi ya
mitandao ya kijamii yanaongezeka kila kukicha na kuleta upinzani kwa
vyombo vya habari. Hii inatokana na ukweli kwamba kupitia mitandao hiyo
habari husambaa kwa haraka katika muda mfupi.
Watu wengi duniani wanatumia mitandao tofauti ya
kijamii huku wanamuziki na wanamichezo wakiongoza katika orodha ya kila
mtandao duniani bila kuwaacha wanasiasa.
Ndiyo maana;‘dunia ilisimama’, baada ya mtandano
wa facebook kutoingilika Jumanne ya Januari 27, mwaka huu. Mamilioni ya
watumiaji wa mtandao huo walikumbwa na wasiwasi wa kuvamiwa kwa mtandao
huo. Kwa muda wa dakika 40, hakuna aliyeweza kuingia katika akaunti yake
asubuhi ya siku hiyo.
Hitilafu hiyo ilisababisha wateja wa mtandao wa
Instagram pia kukosa huduma. Hiyo ni kwakuwa mtandao huo upo chini ya
kampuni ya facebook. Uongozi wa kampuni hiyo ulilazimika kutoa maelezo
ya kilichotokea.
Msemaji wa facebook alikaririwa na Shirika la
Utangazaji Uingereza (BBC) akifafanua juu ya hitilafu za kiufundi
zilizojitokeza ili kuondoa wasiwasi uliokuwepo miongoni mwa wateja wake
kwamba mtandao huo umevamiwa.
Msemaji huyo alibainisha kuwa tatizo
lililojitokeza lilisababishwa na mabadiliko yaliyofanywa na mafundi
kabla ya kuathiri mfumo mzima. Lakini lilitatuliwa baada ya muda mfupi.
Huduma ya mitandao hiyo haikupatikana kwa muda wa dakika 40, duniani
kote.
Hiyo inaonyesha ni kwa namna gani mitandao hii
imekuwa muhimu katika jamii ya sasa. Mchango wake umekuwa muhimu sana
katika maisha ya wanamuziki na wanamichezo bila kuwasahau wanasiasa.
Watu maarufu na mashuhuri hufaidika zaidi.
Wanamuziki na wanamichezo wananufaika zaidi
kutokana na kuwa na wafuasi wengi katika mitandao tofauti ya kijamii.
Idadi hiyo huongeza thamani ya mikataba mbalimbali wanayoingia. Idadi
kubwa ya wafuasi kwa watu hawa ni mtaji wa biashara.
Hata kwa wanasiasa ina maana kubwa. Inaonyesha
vitu viwili vikubwa; mosi, ni kwa namna gani mwanasiasa husika
anakubalika katika jamii yake na pengine duniani kwa ujumla. Pili, ni
kwa kiasi gani anajiweka karibu na wananchi. Mitandao ya kijamii inatoa
fursa kwa mwanasiasa kuwasiliana na wafuasi wake moja kwa moja.
Ingawa wanamuziki ndiyo watu wanaoongoza kwa kuwa
na wafuasi wengi katika mitandao hii duniani kote kwa ujumla, hali ni
tofauti hapa nchini na Afrika Mashariki kwa jumla. Hilo limethibitishwa
na utafiti uliofanywa na jarida la wiki la Mail & Guardian la Afrika
Kusini lililoangalia ufuasi huo kwa Bara la Afrika pekee.
Matokeo ya utafiti
Utafiti huo uliotolewa hivi karibuni, unaonyeshsa
kuwa mwanasiasa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe anaongoza
miongoni mwa Watanzania wanaotumia mitandao hiyo.
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon