 Masanja na mke wake Saumu wameishi kwenye ndoa kwa miaka kumi 
sasa. Hapo awali, kila kitu kilikuwa sawa katika uhusiano wao, lakini 
katika miaka ya karibuni, Masanja amekuwa hana matamanio tena na Saumu
hana hamu kabisa ya tendo la ndoa.
Masanja na mke wake Saumu wameishi kwenye ndoa kwa miaka kumi 
sasa. Hapo awali, kila kitu kilikuwa sawa katika uhusiano wao, lakini 
katika miaka ya karibuni, Masanja amekuwa hana matamanio tena na Saumu
hana hamu kabisa ya tendo la ndoa.
Tatizo hili limekuwa likiwaathiri watu wengi hapa 
nchini na hata duniani kote. Haliwaathiri wanaume pekee kama ilivyo kwa 
Masanja, bali hata wanawake nao hukumbwa na tatizo hilo.
Utafiti uliofanyika nchini Uingereza , Ulaya na 
Marekani, ukijumuisha wanawake wa rika zote, ulibaini kuwa asilimia kati
 ya 30 na 50 ya wanawake wanakumbwa na tatizo la kukosa hamu ya 
kujamiiana.
Wakati huo utafiti huo ukiweka bayana hilo 
kutokana na tatizo la uzazi au kukoma kwa hedhi, tafiti nyingne 
zinaonyesha kuwa karibu robo tatu ya wanawake hawafikii kilele cha tendo
 hilo au wanapata maumivu.
Wataalamu wa afya wanaeleza kuwa kukosa hamu ya tendo la ndoa kunatibika, iwapo hatua muhimu na za msingi zitachukuliwa.
Ni vyema kufika mapema katika huduma za afya ukiwa na mwenza wako kwa ajili ya uchunguzi na matibabu.
Nini suluhisho la kukosa hamu ya kujamiiana
Kwanza kabisa, inashauriwa kitaalamu kubadilisha 
mfumo wa maisha kwa mfano, kubadili ratiba za kazi, matembezi au ratiba 
za wenza.
Kupunguza msongo wa mawazo kwa kukubali kwamba 
tatizo lipo baina ya wanandoa na hivyo kutafuta suluhu pamoja na kuacha 
ugomvi. Matatizo ya kimaisha lazima yatafutiwe ufumbuzi.
Kufanya mazoezi ya misuli ya kiuno kwa kufanya 
kama unazuia mkojo wakati unahisi haja ndogo na kuhesabu kutoka moja 
hadi tano, baada ya tano pumzika na halafu rudia. Haya mazoezi (kegel 
exercise) huongeza uwezo wa kujamiiana kwa wanawake
Kubadilisha mfumo wa maisha kwa wapenzi 
Zungumza na mwenza wako – Malumbano na matatizo ni vitu vya 
kawaida katika uhusiano wowote, ni vizuri kwa wenza kukaa pamoja na 
kuzungumza matatizo yao, kuwa wa kweli, waaminifu, kuaminiana, kujaliana
 na kuzungumza juu ya tendo la ndoa kwa pamoja.
Ni vizuri kila mmoja kuainisha vitu anavyopenda na
 asivyopenda kufanyiwa wakati wa kujamiiana. Pale inapotokea mmoja 
hajapendezwa au kufurahishwa na uwajibikaji au ufanisi wa mwenzie basi 
hana budi kutumia lugha nzuri kutafuta kiini cha tatizo na kulitafutia 
ufumbuzi.
Weka mazingira mazuri na muda wa kufanya tendo la ndoa na mwenza wako ili mpate kudumisha uhusiano wenu.
Ongeza msisimko katika uhusiano wenu kwa kujaribu 
aina au staili mbalimbali wakati wa kujamiiana, kubadilisha muda wa 
kufanya mapenzi (sio usiku tu hata asubuhi, mchana) au sehemu tofauti na
 ile mliyoizoea wakati wa kufanya mapenzi (sio kila siku kitandani).
Kupata ushauri nasaha kutoka kwa wataalamu wa 
mambo ya uhusiano, ndoa na hata madaktari wa magonjwa ya akili kwani 
hawa ni weledi zaidi katika kazi yao.
Tiba ya dawa
Kutibu ugonjwa ambao ni kiini cha tatizo hili – Kisukari, magonjwa ya moyo, magonjwa ya zinaa nk
Daktari kumbadilishia mgonjwa dawa zinazosababisha madhara kama ya msongo wa mawazo na sonona.
Kutibu tatizo la sonona na wasiwasi.
Kutumia dawa au vilainishi vya  ukeni wakati wa tendo la ndoa kwa wale wanaopata maumivu au kupunguza uke kuwa mkavu au kuwasha.
Tiba ya vichocheo (homoni) 
Dawa za kitaalamu za kuongeza hamu au nguvu 
atakuandikia daktari baada ya kufahamu kiini cha tatizo. Haishauriwi 
kutumia bila ushauri wa daktari kwani dawa hizi zina madhara.
Ikumbukwe ya kwamba vyakula hivi sio tiba mbadala bali husaidia 
tu kupunguza ukubwa wa tatizo hili la kupungua au kukosa hamu ya 
kujamiiana na kuboresha kwa wale ambao hawana tatizo hili na hivyo 
kudumisha uhusiano.
Kitunguu swaumu – Kitunguu swaumu kina kemikali 
ambayo huongeza mzunguko wa damu kwenda kwenye uume, huongeza hamu ya 
kufanya mapenzi na utolewaji wa mbegu za kiume.
Habat al soda – Mafuta, mbegu, au unga wa habat 
soda kama wengi wanavyoiita na ambazo zimetumika kwa miaka mingi sana 
kupunguza tatizo hili na waandishi wengi wa tiba ya nguvu za kiume  
wameeleza umuhimu wake. Tumia kidogo kwenye chai au maji ya uvuguvugu 
mara mbili kila siku. Mbegu hizi hupatikana kwa wingi katika nchi za 
asia kama Saudi Arabia, Syria, Iran, Dubai (UAE), na hata Misri, 
Tanzania-maeneo ya pwani hupatikana.
Giligilani – Hii huchochea hamu ya tendo la ndoa kutokana na uwepo kwa wingi wa kichocheo aina ya androsterone.ina ya androsterone.
Ndizi – kuwepo kwa wingi kwa kimeng’enyo aina ya 
‘bromelain’ na madini  ya potashiam, huongeza msisimko wa tendo kwa 
wanaume. Potassium pia hupatikana kwenye tikiti maji ambalo pia lina 
kemikali aina ya ‘arginine’  ambayo huongeza wingi wa damu katika 
mishipa ya damu na hivyo kusaidia katika kusimika kwa uume. 
Parachichi – Huwa na kiwango kikubwa cha madini 
ya  folic acid ambayo huvunjavunja protini. Vitamini B6 kwenye 
parachichi huchochea kutengeza vichocheo vya kiume kwa wingi.
Mayai – Mayai yana kiwango kikubwa sana cha 
vitamini aina ya B5 na B6, ambazo husaidia kuleta usawa wa viwango vya 
vichocheo mwilini na kupunguza msongo wa mawazo.
Nyanya – Zina kiwango kikubwa cha virutubisho  
aina ya bio-active phyto-nutrients, lycopene, na beta carotene ambazo 
husaidia kuleta damu kwa wingi kwenye uume na hivyo kusaidia kusimika 
kwa uume
‘Chocolate’ – Ina kiwango kikubwa cha kemikali ambazo huongeza hamu ya tendo.
Vitamin A – Husaidia katika kuweka usawa wa 
vichocheo vya mapenzi. Vyakula venye wingi wa vitamin hii ni pamoja na 
karoti, maini,tikiti  maji, spinach, maziwa nk.
Vitamin B complex – Huongeza kiwango cha kichocheo cha testerone
 ambacho husaidia katika kuongeza ufanisi wa tendo la ndoa kwa wanaume 
na wanawake. Vitamini B complex hupatikana kwa wingi kwenye ndizi, viazi
 tamu, lentils mboga za majani, parachichi, mayai, samaki aina ya jodari
 (tuna), bata mzinga, maini nk.
Mdalasini na Asali– Mchanganyiko wa vitu hivi viwili husaidia sana katika kuongeza ufanisi kwa wale wenye tatizo hili.
Sign up here with your email
 
ConversionConversion EmoticonEmoticon