Mpango wa Zitto kuondoka CHADEMA na wabunge 3 wagundulika




Taarifa ambazo bado hazijathibitishwa zinasema kuwa kuna wabunge watatu wa chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA wanatarajiwa kujitoa ndani ya chama hicho mwishoni mwa mwezi huu na kujiunga na chama cha ACT.
Taarifa hizo zinasema pia hii ni baada ya majadiliano ya muda mrefu na kufikia muafaka na mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe anayetarajiwa kuongoza wabunge hao watatu kujiunga na chama hicho katika mkutano mkuu wa ACT tarehe 28/3
Taarifa zaidi zinasema pia kuna wabunge wachache wa CCM na NCCR waliofikia muafaka wa kumuunga mkono Zitto kwenda ACT ingawa idadi yao haijajulikana.
Taarifa zaidi zinasema kuna mjumbe mmoja wa Kamati Kuu CHADEMA anatarajiwa pia kuungana na kundi hili kwenda ACT.
Wabunge hao wa Chadema inadaiwa ni wale mizigo ambao hawana ushawishi wowote ndani ya chama hicho na ambao wana uhakika hawawezi kupitishwa tena kugombea.
Tunatarajia kuwawekea hapa majina yote kamili siku chache zijazo baada ya uchunguzi wetu kukamilika kwani tuna vyanzo vyetu vya habari ndani ya mazungumzo hayo ingawa ni ya siri sana.
Zitto Kabwe amekuwa akikaririwa mara kadhaa kusema hatma yake kisiasa ataitangaza mwezi huu

Previous
Next Post »