Copy and WIN : http://bit.ly/copynwin
SERIKALI imetoa taarifa rasmi kuhusu uhalifu uliotikisa mkoani Tanga,
ikisema hali ni shwari na umma wa Watanzania upuuze taarifa
zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zikitia hofu.
Aidha, imesema watu kadhaa wanashikiliwa wakihusishwa na uhalifu huo.
“Tunawashikilia ila mpaka sasa siwezi kukueleza idadi yao na kwamba ni
wa kikundi cha ugaidi au la.
Hao watu tunafanya nao mahojiano ili kuweza kuelewa kama wanahusika
kwenye tukio hilo,” alisema Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga,
Juma Ndaki.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari, Ndaki alisema hali katika
kitongoji cha Majimoto, Amboni na mkoa wa Tanga kwa ujumla iko shwari.
“Tunaendelea kufanya uchunguzi kubaini hao wahalifu pamoja na silaha
zilizoibwa,” alisema.
“Tunaomba wananchi waendelee kutoa ushirikiano wao hasa wanapoona watu
wenye majeraha au wanaowahisi kwamba ni wahalifu ili nasi tuweze
kuwachunguza kama wanahusika kwenye tukio hili”, alisema.
Ingawa Kamanda hakuelezea mazingira ya kukamatwa kwa watuhumiwa,
waandishi wa habari waliozuru eneo la Amboni yalikotokea mapigano,
waliarifiwa kwamba baadhi ya wavuvi kwenye Mto Zigi, walimkamata mtu
wakimtuhumu kukutwa akifua nguo zenye damu.
Katika mapigano hayo baina ya askari na wahalifu, yalisababisha kifo cha
askari wa JWTZ, Sajenti Said Kajembe na wengine kujeruhiwa.
“Asubuhi wavuvi kadhaa walikuwa hapo mtoni ghafla walikutana na mtu
pembeni ya mto akiwa anafua kanzu pamoja na vifaa fulani kama nguo za
kufunika uso ..’maski’ ikabidi wawapigie haraka polisi simu lakini
hawakuweza kupatikana na ndipo wakawapigia askari wa JWTZ ambao walifika
haraka eneo la tukio na kumkamata mhusika”, alisema mkazi mmojawapo.
Ulinzi waimarishwa Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Magalula Said
Magalula aliwataka wakazi wa Tanga na vitongoji vyake, kuondoa hofu kwa
kuhakikisha wanaendelea na shughuli zao za uzalishaji kwa sababu ulinzi
umeimarishwa na hali ya usalama ni shwari.
Pia, aliwataka wananchi na wageni wenye mpango wa kutembelea eneo la
kihistoria la Mapango ya Amboni, kuendelea na ratiba zao kwa sababu eneo
hilo liko salama na tangu awali halikuhusika kwenye vurugu hizo.
Magalula ambaye pia alikutana na waandishi wa habari, alisema “Hali ni
nzuri ulinzi na usalama uko imara… naomba wananchi waondoe hofu, wawe na
amani na waendelee na shughuli zao za uzalishaji… hakuna tatizo kabisa
usalama umedhibitiwa vizuri.”
Mkuu huyo wa mkoa ambaye Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya
Mkoa, alisisitiza “Naomba Watanzania wenzangu muelewe kwamba eneo
lilipofanyika tukio la mapigano na wahalifu si pale yalipo mapango ya
Amboni ... maeneo hayo yapo mbali na nitoe mwito kwa wageni wenye mpango
wa kutembelea hapo wawe huru kufanya hivyo mahali hapo ni salama.”
“Naomba Watanzania nchini kote kwa ujumla wawe na amani kwa sababu Tanga
iko shwari hakuna tena hizo vurugu za wahalifu… naomba wasiamini sana
taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii… sisi tuko shwari na
shughuli za kijamii zinaendelea kama kawaida ikiwemo Amboni,” alisema.
Akizungumzia mapigano hayo yaliyotokea Februari 14, alisema licha ya
majibizano ya kurushiana risasi yaliyofanywa na askari wa Polisi kwa
kushirikiana na wa JWTZ , uchunguzi unaendelea kuwapata wahusika.
“Vikosi vya usalama vinaendelea na juhudi za kuwasaka pamoja na kutafuta
silaha zetu lakini hakuna mtu yeyote anayeshikiliwa … zipo simulizi
mbalimbali zinazoendelezwa kwenye mitandao ya kijamii ila sisi serikali
ya mkoa bado hatujathibitisha kwamba watu hao ni wa kikundi gani ila
ninachokifahamu hao watu ni wahalifu”, alisisitiza.
Kuhusu kuongezeka kwa matukio katika maeneo mbalimbali mkoani humo,
alisema kila tukio linachukuliwa kwa uzito mkubwa na linashughulikiwa
kwa namna linavyotokea.
Aidha, aliwataka wakazi wa Tanga hususan wanaoishi eneo la Amboni na
vitongoji vyake kuhakikisha wanaendelea kutoa habari sahihi kuhusu watu
mbalimbali wanaowatilia shaka .
Alisema taarifa hizo zina umuhimu wa kipekee kwa askari katika
kufanikisha kukamatwa kwa wahalifu hao. Zakutwa nguo, vyombo Kutokana na
maswali mengi ya wanahabari na wananchi, kudai kutoridhishwa na
mwenendo wa utoaji taarifa kuhusu tukio hilo, Mkuu wa Mkoa aliruhusu
watembelee eneo la tukio kuthibitisha kama hali ni shwari katika eneo
husika.

husika
Copy and WIN : http://bit.ly/copynwin
Copy and WIN : http://bit.ly/copynwin
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon