Bony, Yaya Toure wafutwa Man City


KOCHA Manuel Pellegrini amesema Yaya Toure na Wilfried Bony hawatacheza dhidi ya Stoke City kwenye Ligi Kuu England Jumatano hii licha ya kwamba watakuwa wamemaliza majukumu yao kwenye michuano ya Afcon 2015 walipokuwa na kikosi chao cha Ivory Coast.  Mastaa hao jana Jumapili walitarajia kucheza fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya Ghana mjini Malabo, Guinea ya Ikweta, lakini kocha wao klabuni Manchester City alisema hawatarudi na kucheza katika mechi ya Ligi Kuu itakayofanyika katikati ya wiki hii.  “Hatuwahitaji wote hao kurudi haraka kikosini, haiwezekani kucheza mechi ya Jumatano dhidi ya Stoke,” alisema Pellegrini.  Pellegrini alisema pia hana wasiwasi juu ya hali ya usalama kwa nyota wake hao wanaoshiriki fainali za Afcon nchini Guinea ya Ikweta, ambako jana ilielezwa usalama kuimarishwa zaidi ili kuepuka kilichotokea kwenye mechi ya nusu fainali kati ya Ghana na wenyeji hao ambapo mashabiki walifanya fujo zilizosababisha mechi kusimama kwa karibu dakika 20.  “Baada ya mechi hiyo tutakuwa na siku 10 bila ya mechi na nadhani kwa kipindi hicho watakuwa wamerudi kwenye kikosi,” alisema.
Previous
Next Post »