SIRI: Mambo ya nyuma ya pazia

KIUNGO Frank Domayo huenda maisha yake ya soka yangekwisha miezi michache ijayo kutokana na jeraha kubwa alilokuwa nalo katika paja lake wakati akiwa Yanga. Hakuna aliyejali hilo pale Yanga na kumwacha aendelee kucheza na majeraha hayo.  Azam ilionekana kujali na kumpeleka Domayo kufanyiwa upasuaji Afrika Kusini mara tu baada ya kumsajili na sasa ameanza kurejea katika makali yake ya awali. Ni jambo la kipekee.  Kitendo walichokifanya Azam kwa Domayo ni miongoni mwa mambo mengi yanayoitofautisha timu hiyo na klabu za Simba na Yanga. Mambo mengi wanayofanya yamekuwa ya kipekee na kuipa heshima klabu hiyo.  Makala haya yanazungumzia mambo kadhaa ya nyuma ya pazia katika klabu hiyo tajiri zaidi nchini
Previous
Next Post »