LIGI kuu soka Tanzania bara imeendelea kwa mechi tatu kupigwa leo.
Uwanja wa
CCM Kambarage Shinyanga, bao pekee la Rashid Mandawa katika dakika ya
38' kwa shuti kali la mguu wa kushoto limewapa ushindi wa 1-0 Kagera
Sugar dhidi ya Polisi Morogoro.
Kwa matokeo hayo, Kagera Sugar wamefikisha pointi 24 katika nafasi ya tatu baada ya kushuka dimbani mara 16.
Pia Mandawa amefikisha mabao 7, bao moja nyuma ya mfunga anayeongoza orodha ya wafungaji, Didier Kavumbagu.
Huku Nangwanda Sijaona Mkoani Mtwara, Ndanda fc imeifumua bao 1-0 Coastal Union.
Bao la
ushindi la Ndanda limefungwa na Jacob Masawe katika dakika ya 74'
akimalizia mpira wa adhabu ndogo uliopigwa na Paul Ngalema.
Kwa
matokeo hayo, Ndanda fc wamefikisha pointi 19 kufuatia kushuka dimbani
mara 16 na wamepanda nafasi moja na sasa wamekuwa wa 10 nyuma ya Polisi
Moro wenye pointi 19, lakini wana wastani mzuri wa mabao ya kufunga na
kufungwa.
Mbeya City sasa wameshuka mpaka nafasi ya 11, wakisubiri mechi yao ya kesho dhidi ya Yanga.
Mechi nyingine ilipigwa uwanja wa CCM Mkwakwani Tanga ambapo Mgambo JKT imeifunga bao 1-0 Coastal Union ya Tanga.
Kwa
matokeo hayo, Mgambo wamefikisha pointi 17 katika nafasi ya 12, wakati
Coastal Union wameendelea kubakia nafasi ya 7 wakijikusanyia pointi 19
baada ya kushuka dimbani mara 16.
Ligi hiyo itaendelea kesho mwa mechi tatu kushika kasi.
Mbeya
City watakuwa nyumbani kuwakaribisha Yanga uwanja wa Sokoine, Simba
watakuwa wageni wa Stand United uwanja wa CCM Kambarage Shinyanga,
wakati Azam fc watakabiliana na Tanzania Prisons uwanja wa Azam Complex.
Mechi hii itapigwa usiku
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon