Sign up here with your email
HONGERA SANA MTU WA NGUVU MILLARD AYO.......CHEKI ALICHOFANYA
Mtangazaji wako wa nguvu,Millard Ayo mfanyakazi wa Clouds Fm kipindi cha
Amplifier amefungua studio kubwa ya kisasa iliyomghalimu mamilioni ya
shilingi."Ilikuwa si kazi ndogo kuanzisha hii studio ambayo nimeijenga
mwaka mmoja kwa kudunduliza kihasi kidogo kidogo ninachokipata" alisema
Millard Ayo.
Ameandika hivi kwenye ukurasa wake wa Facebook:
"Siku zote ni furaha pale ndoto inapokua kweli, nilitamani sana siku
moja Millard Ayo kumiliki studio yangu ya Radio kutokana na jasho langu
na leo Namshukuru Mungu nimefanikiwa kumaliza ujenzi wa studio yangu
baada ya kudunduliza kidogokidogo kwa zaidi ya mwaka mmoja ndio maana
hata wewe hutakiwi kukata tamaa kwa chochote hata kama kinachelewa mtu
wangu, nilianza kuidizaini hii na baadae watu wangu @francis_ayo na
@abdul8819 wa @pixelbasetz wakanisaidia sana yani, nina mengine yanakuja
ila kwa leo nimekupa hii tu mtu wangu! hapa panaitwa #TZA !! thanks
kwa Maboss wangu Joe Kusaga, Ruge na @sebamaganga wamenipa nguvu na
nafasi kubwa sana kwenye maisha yangu! birthday yangu ilikua Jan26 na
nimejipa hii studio kama zawadi kubwa kwenye maisha yangu baada ya
kuihangaikia usiku na mchana bila kukata tamaa"

ConversionConversion EmoticonEmoticon