HII ni kali ya mwaka! Staa wa sinema za Bongo, Chuchu Hans amejikuta
akizirai ndani ya jeneza wakati akiigiza sini ya kifo kwenye filamu,
Amani limeinyaka
Staa wa sinema za Bongo, Chuchu Hans akiwa kwenye jeneza.Chuchu
alikumbwa na hali hiyo hivi karibuni akiwa ‘lokesheni’ ya kuigizia
filamu hiyo maeneo ya Mbezi ya Kimara jijini Dar es Salaam ambapo
sanjari na yeye, msanii mwingine aliyecheza nafasi ya mwanakwaya naye
alipoteza fahamu wakati kipande hicho kikirekodiwa.
TATIZO UHALISIA, WASIWASI
Chanzo kimoja kutoka ndani ya kundi la wasanii waliokuwa wakiigiza
filamukinasema kuwa, Chuchu alikumbwa na hali hiyo kutokana na wasiwasi
na ujasiri wa kuuvaa uhusika.“Awali, Chuchu alionesha wasiwasi wa
kuigiza kipande hicho cha kumwonesha yeye yumo ndani ya jeneza akiwa
amefariki dunia kwa ugonjwa kama wa kichaa kilichotokana na msongo wa
mawazo baada ya kubakwa.
“Mbaya zaidi, mwongozaji naye alisema ni lazima akiwa amelala ndani ya
jeneza awekewe pamba za kuziba matundu ya pua kama maiti wanavyowekewa,”
kilisema chanzo....Waombolezaji wakilia kwa uchungu.
ILIKUWA WAKATI AKIAGWA
Chanzo kikazidi kudai kwamba, taharuki yote hiyo ilitokea pale, ‘mwili’
wa Chuchu ukiagwa kwenye Kanisa la Sabato, Mbezi, Dar ambapo
waombolezaji walipokuwa wakipita, binti yake, Farha (9) aliangua kilio
kilichomfanya Chuchu ajikute akikata pumzi ghafla!
AMALIZA SINI, ASHINDWA KUAMKA
Ikaelezwa kwamba, ilikuwawakati kipande hicho kimeisha huku binti yake
akiendelea kulia kwa kumwona mama yake ndani ya jeneza, Chuchu hakuamka
ili kuendelea navipande vingine hali iliyowafanya watu wazima kumkagua
na kugundua alizirai.“Watu walianza kupagawa, wengine walijua
ameshapoteza maisha. Lakini Mungu mkubwa Chuchu akazinduka na kumkuta
mwanaye bado akilia kwa nguvu. Ilibidi wasanii wengine waingilie kati
kumtuliza,” kilisema chanzo.Waombolezaji wakiwa na simanzi.
MWINGINE AITIWA MCHUNGAJI
Wakati Chuchu ‘akifufuka’, yule msanii aliyeigiza nafasi ya mwanakwaya
yeye alikuwa bado chini amelala chali akiwa hajitambui kwa kile
kilichokuwa kikiendelea.“Yule mwenzake ilibidi aitwe mchungaji wa kanisa
hilo ambaye alikuwa jirani kwa ajili ya kumwombea japo mchungaji wa
filamu hiyo alikuwa ni msanii Jimy Mafufu,” kilisema chanzo.
MASWALI ENEO LA TUKIO
Baadhi ya wasanii walianza kujiuliza nini kilisababisha hali ile
kwaniilionekana kama kuna roho chafu aliyetaka kufanya mauaji ya
makusudi.“Wengine waliuliza kama kuna mtu ana vitu kama hirizi au chanjo
ya mamboya kishirikina, ikaonekana hakuna. Lakini maswali yalikuwa
mengi sana,” kilisema chanzo.
Jeneza likiandaliwa kwa ajili ya mazishi.
CHUCHU AONGEA NA AMANI
Baada ya kuinasa taarifa hiyo, Amani lilimsaka Chuchu kwa njia ya simu
yake ya mkononi na kumuuliza ambapo alikiri kutokea kwa tukio hilo.Huyu
hapa: “Yaani siwezi kueleza juu ya ile filamu maana ilikuwa ni hatari
tupu na sijui hata mama yangu akiiona itakuaje kwakweli.“Lakini kwenye
ile sini yangu ndiyo ilikuwa ikihitaji hivyo, nilale kama maiti kweli na
huwezi amini lilichimbwa hadi kaburi la ukweli. Mimi nilizimia si chini
ya mara moja. Pumzi yangu ilikata hasa nilipomsikia mwanangu akilia.”
CHUCHU ANAWEZA ASIWE SAWA KISAIKOLOJIA
Kwa mujibu wa maswali yakisaikolojia kwa wasanii wamaigizo, baada ya
msanii kuigiza filamu inayohusu ukatili wowote, kumwaga damu, mapenzi ya
kupitiliza, kifo au jambo lolote ambalo ni chungu kwa ubinadamu ni
lazima aombewe na viongozi wa dini ili kuifukuza roho hiyoya
kuigizia.Wanasaikolojia wanasema kuwa, msanii akiigiza nafasi kama hizo
na kujiacha hivihihivi kuna hatari baada ya muda kuambukizwa na uigizaji
huo ikawa ndiyo maisha yake ya kila siku. Ndiyo maana baadhi ya wasanii
wa filamu duniani kote wanaishi maisha ya sawasawa na wanavyocheza
filamu.
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon