Cristiano Ronaldo amekuwa mchezaji wa tatu kwa kuifungia Real Madrid magoli mengi zaidi baada ya kufikisha mabao 290 wakati klabu yake ikiichapa Elche 2-0 katika mchezo wa La Liga Jumapili usiku.
Ushindi
huo umeikita Real Madrid kileleni kwa pointi nne safi mbele ya
Barcelona ambayo iliteleza Jumamosi kwa kukubali kipigo cha 1-0 kutoka
kwa Malaga.
Kwa
kutupia wavuni magoli 290, Ronaldo analingana na Santillana huku
Alfredo Di Stefano akishika nafasi ya pili kwa kufunga magoli 305 wakati
Raul anaongoza kwa magoli 323.
Wakati Santillana alifunga magoli 290 katika mechi 645, imemchukua Ronaldo mechi mechi 281 tu kufikisha idadi hiyo.
Goli lingine la Real Madrid lilifungwa na Karim Benzima wakati kocha Carlo Ancelotti akifikisha kwa ushindi mchezo wake wa 100 wa kuikochi timu hiyo.
Kipa
Iker Casillas naye alikuwa na cha kujivunia katika mchezo huo baada ya
kumaliza mchezo wake wa 500 kwa Real Madrid kwa ushindi muhimu huku
lango lake likiwa halijaguswa.
Elche
(4-4-1-1): Tyton; Suarez, Roco, Lomban, Edu Albacar; Rodriguez, Adrian (
Herrera 81), Pasalic (Galvez 75), Niguez (Mendes Rodrigues 64) ; Fajr;
Jonathas.
Real
Madrid (4-3-3): Casillas; Carvajal, Pepe, Varane, Marcelo; Lucas Silva
(Illarramendi 84), Kroos, Isco (Arbeloa 89); Bale, Benzema (Jese 93),
Ronaldo.
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon