Diamond
Platnumz ni miongoni mwa marafiki wa karibu wa msanii Dully Sykes ambaye
weekend iliyopita alimpoteza baba yake mzazi Ebby Sykes, lakini
hakuweza kuhudhuria msiba huo kutokana na sababu ambazo amezitoa leo.
Diamond
ambaye wakati msiba huo unatokea alikuwa Zanzibar na mpenzi wake Zari,
ameelezea sababu zilizomfanya kushindwa kuhudhuria mazishi.
“Watu waliniona niko zanzibar lakini walikuwa hawajui nimeenda kufanya nini,” Diamond
ameiambia 255 ya XXL ya Clouds FM. “Usiangalie kila unachokiona Instagram ukajua mtu labda kwasababu alikuwa anafanya starehe.
Niko
katika kipindi ambacho sio kizuri kwangu mimi na familia yangu kwasababu
kuna vitu ambavyo siwezi kuvizungumza lakini, na siwezi kuviweka kwenye
media ndo maana watu wengine wanaweza kuniona nacheka lakini […kwanza
mama yangu anaumwa na anaumwa sana sijawahi kulizungumza hili ndo
nalizungumza hapa, hapa ninapoongea na wewe yupo India, kuna vitu vingi
vinaendelea, siwezi kusema nilikuwa Zanzibar nafanya nini
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon