Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa ya
Njombe, imemhukumu aliyekuwa mkuu wa kituo cha Polisi Ilembula kifungo
cha miaka 30 jela, baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka mtuhumiwa
aliyekuwa ndani ya mahabusu.
Hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu
Augustine Rwezile, baada ya mshtakiwa huyo James Nyambenga kukiri kosa
hilo mahakamani, ambapo mshakiwa huyo anadaiwa kumtoa msichana huyo
kwenye chumba cha mahabusu alikokuwa anashikiliwa na kumbaka.
Mwanamke huyo ambae ni mhudumu wa bar alikuwa anashikiliwa kwenye mahabusu ya kituo hicho kwa tuhuma za uzururaji.
Akisoma hukumu hiyo Hakimu
Rwezile amesema ushahidi uliotolewa na upande wa mlalamikaji na
vielelezo vya daktari aliyempima msichana huyo viliweza kuithibitishia
Mahakama kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo.
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon