Imevuja! Kuna madai kwamba staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ametupiwa jini lakini likamkosa na kumpata mama yake mzazi, Sanura Kassim ‘Sandra’ kisha kumsababishia ‘gonjwa’ la ajabu, Ijumaa Wikienda linakupa mchapo kamili.
Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na mama yake mzazi, Sanura Kassim ‘Sandra’.
TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa
mujibu wa chanzo makini, watu wanaodaiwa kuwa ni wabaya wa Diamond
(Anti-Diamond) walimtupia jini staa huyo lakini bahati nzuri likamkosa
na kwa bahati mbaya likampata mama yake ambaye alipata ugonjwa wa
kupooza ghafla.
“Ujue kumekuwa na sintofahamu kwa muda mrefu juu ya ugonjwa wa mama Diamond lakini habari za uhakika ni kwamba, mama Diamond yupo hoi baada ya kutupiwa jini ambalo mlengwa wake alikuwa Diamond.
“Mungu tu hakupenda limpate Diamond lakini inasemekana kwamba jini hilo
ni hatari endapo lingempata Diamond kwa jinsi lilivyokuwa, basi pengine
leo tungekuwa tunazungumza mengine,” kilisema chanzo hicho.
DIAMOND ALIJUA ‘MCHEZO’ HUO?
Chanzo
hicho kilizidi kumwaga data kwamba, Diamond alijua kwamba mama yake
ametupiwa jini ndiyo maana alikuwa akisuasua kutoa uamuzi wa kumuwahisha
nchini India kwa matibabu ya hospitali.
“Diamond
alijua kuhusu mpango huo wa wabaya wake kutaka kummaliza kishirikina
ndiyo maana hakutaka kumkimbiza haraka hospitali na badala yake
alijikita kwenye swala na dua kwani yeye anaamini katika dini zaidi,”
kilisema chanzo hicho.
Hata
hivyo, baada ya kutafakari kwa umakini wa hali ya juu, imeelezwa
kwamba, Diamond alilazimika kumpeleka mama yake nchini India na kupatiwa
matibabu kisha kurejea nchini.
ALIRUDI MZIMA
Kwa
mujibu wa ndugu wa Diamond ambaye hakupenda jina lake lichorwe
gazetini, hivi karibuni (kabla ya Valentine’s Day), mama Diamond
alirejea nchini akiwa na afya njema lakini siku chache baadaye alizidiwa
tena na kurudishwa India huku ndugu wakijawa na hofu.
“Alirudi Bongo lakini hakukaa sana akazidiwa tena tukalazimika
kumrudisha India kwani hali ilizidi kuwa mbaya. Tumekuwa hatutaki
kueleza sana juu ya suala hili maana Diamond mwenyewe hapendi haya mambo
yajulikane,” alisema ndugu huyo.
DIAMOND AFUNGUKA
Baada
ya chanzo hicho kuvujisha ‘ubuyu’ huo, mwanahabari wetu alimvutia waya
Diamond ambapo alikiri kwamba mama yake yupo India lakini hakutaka
kulizungumzia zaidi eneo hilo badala yake akaanza kushusha lawama kwa
wale aliodai wanamsema vibaya.
“Mama
bado yuko kwenye matibabu nchini India na hali yake kusema kweli si
nzuri, naomba hapo nisizungumzie sana. Kuhusu masuala ya kutupiwa jini,
mimi namuamini Mungu, naamini mama atapona.
“Inaniuma
kila siku ninaposikia watu wanaongea vitu ambavyo si kweli na kwa namna
nyingine nashindwa kujibu vitu ambavyo mwenyewe sivijui hivyo yote
namwachia Mungu, maana yeye ndiye jibu la yote.
“Halafu pia kuna muda ufike, watu wawe wanafahamu mimi pia ni binadamu
kama binadamu wengine, wasiwe wananijazia vitu utafikiri mimi sina moyo,
wawe waelewa, sipo katika kipindi kizuri kwa sasa na si kila kitu
wanachosikia au kuona lazima mimi nikizungumzie, kuna mambo mengine ni
ya ndani ya ukoo na yako juu yangu sana, hivyo ukiona kimya simaanishi
kuna watu nimewadharau,” alisema Diamond.
TUMEFIKAJE HAPO?
Hivi
karibuni kuliibuka madai kwamba kwa makusudi Diamond alishindwa
kuhudhuria msiba wa baba Abdul Sykes ‘Dully’ na badala yake picha
zikavuja zikimuonesha akiwa kisiwani Zanzibar na mpenzi wake Zarina
Hassan ‘Zari’ kitu ambacho mwenyewe alikikanusha.
“Si kila picha unayoiona katika mtandao wa kijamii basi itakuwa imepigwa
muda huo, inaweza kuwekwa leo kumbe ni ya muda mrefu,” alisema Diamond.
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon