MKONGWE wa muziki wa kizazi kipya nchini, Abdul
Sykes maarufu kama Dully, Jumapili usiku alikesha akilia kiasi cha
kushindwa kupokea simu kutoka kwa wadau mbalimbali waliompigia ili kumpa
pole kwa msiba wa baba yake mzazi, Abby Sykes.
Mkongwe wa muziki wa kizazi kipya nchini, Abdul Sykes maarufu kama Dully akiwa mwenye huzuni kubwa baada ya kufiwa na baba yake.
Mzee Sykes (63) alifariki akiwa hospitalini Muhimbili usiku wa Jumamosi na alitarajiwa kuzikwa Jumatatu jioni.
Muda mwingi Dully alikuwa analia na kuna simu nyingi alishindwa
kupokea, hasa za watu ambao alikuwa hajawasevu katika simu yake.
Isingekuwa rahisi kwake kujibu kila aliyepiga kwa sababu wangeendelea
kumliza, alisema msanii mmoja aliyekuwa karibu na msanii huyo wakati
gazeti hili likimtafuta ili kumpa pole.
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon