Simba yaitangazia vita Stand

TIMU ya Simba SC, imeichimba mkwara Stand United ijiandae kula kichapo kwenye mchezo wa ligi kuu utakaopigwa katika Uwanja wa Kambarage, Shinyanga, Jumapili ijayo.Stand waliwashangaza Simba kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa Uwanja wa Taifa, mwaka jana, baada ya kutoka sare ya bao 1-1.
Akizungumza na Championi Jumatano, Ofisa Habari wa Simba, Humphrey Nyasio, alisema kwa sasa timu hiyo imedhamiria kufanya makubwa ambapo kila atakayekuja mbele yake atapata kibano.
“Tumedhamiria kufanya makubwa kutokana na kikosi chetu kwa sasa kuwa kwenye morali ya ushindi, tunakwenda kupambana na Stand United, wanatakiwa kujiandaa kupokea kipigo na si kitu kingine, hakika tupo vizuri sana,” alisema Nyasio.
Simba ipo nafasi ya nne baada ya kujikusanyia pointi 20 kutokana na kucheza michezo 14 huku Stand wakiwa katika nafasi ya 12 baada ya kukusanya pointi 15 kwenye michezo 15
Previous
Next Post »