Picha mbalimbali zikimuonyesha Diamond na Zari kwenye viunga vya Forodhani visiwani Zanzibar.
Na Andrew Chale wa Modewji blog, Zanzibar
Katika
kile kinachoelezewa na wengi kupitia mitandao ya kijamii na baadhi ya
watu walioongea na mtandao huu wa http://www.bekamtanzania.com/
kupitia http://www.bekamtanzania.com/, na
Modewji blog wamefunguka juu ya kitendo cha mwanamuziki nguli Nchini, Naseeb Abdul
‘Diamond Platnumz’ kutinga visiwani Zanzibar akiwa na wapambe wake
pamoja na Boss Lady Zari ‘asali wa moyo wake’ ni mbwe mbwe za kumzima
Ali Kiba ambaye alitikisa vilivyo katika shoo yake kwenye tamasha la
Sauti za Busara 2015.
Wadadisi wa mambo ukiwemo mtandao huu wa http://www.bekamtanzania.com/
na Modewji blog ambao ulikuwa visiwani humo katika tamasha hilo la 12, la Sauti za
Busara 2015, mji mzima wa Zanzibar kila kona ilikuwa ni habari ya Ali
Kiba, ambaye aliweza kutikisa jukwaa la Sauti za Busara vilivyo ikiwemo
kuimba nyimbo zaidi ya 12, akiimba ‘live’ bila kutumia ‘CD’ ama ‘play
back’ kama wafanyavyo wasanii wengi hasa wa Tanzania.
Ali
Kiba alipiga shoo hiyo Februari 12, kwenye siku ya kwanza ya tamasha
hilo kubwa la saba kwa Bara la Afrika, linalokuza muziki duniani kote.
Kwa
kile kilichoelezewa kuwa alifika kuzima mbwe mbwe za Ali Kiba, ni pale
Diamond na Zari walipotimba viunga vya Forodhani na kisha kuanza kufanya
utalii wa ndani kwa kuangalia vyakula mbalimbali vikiwemo vya baharini
‘sea food’, vyakula vya asili vya kisiwa hicho na vyakula vingine,
ambapo watu walipowashtukia kuwa ni Diamond na Zari, umati wa watu
wakawa wanawafuata nyuma huku wakitaka kupiga naye picha.
Hatua
hiyo ilifanyaa eneo hilo la Forodhani kuwa dogo kwani ghafla mastaa hao
wakaanza kuwekewa ulinzi na wapambe wao ili watimize kile wanachotaka
na kilichowaleta hapo. “Kama unavyowajua Wazanzibar walivyo ‘ngangari’
licha ya kuzuiwa kumsogelea Diamond, lakini waliweza kufanya kile
kinachoitwa ‘Ngunguri’ na kupenya hadi kupiga naye picha kitendo
kilichomfanya Diamond kukubali matokeo.
Tukio
hilo lililodumu kwa muda wa zaidi ya dakika 15, mpaka Diamond na
wapambe wake wanapotea kwenye viunga hivyo, Watu mbali mbali hususani
wanawake walikuwa wakifurika kwa wingi kwa lengo la kumuona na hata
kupiga naye picha.
Ali Kiba akitoa burudani tamasha la Sauti za Busara 2015.
Hata
hivyo, baadhi ya watu waliomkosa pamoja na baadhi ya waliomshuhudia
eneo hilo la Bustani, walibainisha kuwa, Diamond alikuja kuzima upepo
wa Ali Kiba.
“Ali
Kiba, katikisa sana Sauti za Busara kwenye shoo yake hakuna
anayemfikia, ujio wa Diamond amekuja kupima upepo tu si bure” alisema
Bayu, mmoja wa wadau wakubwa wa muziki wa kizazi kipya, Bongo fleva.
Mbali
na Bayuu, wengine walianza kuibua mijadala ya hapa na pale wakihoji
ujio wa Diamond kwani kwa sasa wamekuwa na ‘bifu’ na Ali Kiba licha ya
wote kukanusha kwa nyakati tofauti huku kubwa likiwa nani mkali zaidi.
Kwani
bifu lao hilo pia lilipelekea kila wawili hao wanapopiga shoo ya
pamoja, mmoja wapo kuzomewa ama kutupiwa mawe, hali iliyomkutana Diamond
zaidi ya mara mbili katika shoo tofauti ambazo walikutanishwa steji
moja kwa kile kinachoelezwa kuibuka kwa makundi ‘#Teamkiba’ na
#TeamDiamond’.
Umati wa wadau kutoka kila kona ya dunia waliohudhuria tamasha la Sauti za Busara 2015.
Hata
hivyo, siku hiyo hiyo ya Diamond ambayo alikanyaga visiwani hapo, pia
Ali Kiba alikuwa na shoo nyingine binafsi ya siku ya wapendanao, ambapo
ilisemekana wapambe wa Diamond walienda kupima ‘upepo’ wa jamaa huyo Ali
Kiba.
Hivyo,
kama ilivyo kawaida yake, Diamond, aliweza tupia picha mbalimbali ya
matukio yaliyotokea visiwani humo, huku kikubwa akiwa na Boss Lady Zari
wakitanua raha. Diamond alimwelezea Zari kuwa ndio mara yake ya kwanza
kukanyaga visiwani humo hivyo kwa kiasi kikubwa ‘alikuwa mshamba’ kwani
mtandao huu ulishuhudia boss lady huyo akiangalia kila chakula kwenye
viunga vya Forodhani huku baadhi ya vyakula akionesha kuviogopa.
Katika
hatua nyingine, Mastaa mbalimbali kwa muda wa wiki moja waliweza
kuiteka Zanzibar ikiwemo kwenye tamasha la Sauti za Busara. Mastaa hao
wakiwemo wanamichezo, wanamuziki, wasanii, modoz, designers kwa pamoja
walikuwa wakirandaranda kwenye viunga vya Zanzibar.
Diamond na Boss Lady Zari wakiwa katika pozi za kimahaba kwenye hoteli waliyofikia visiwani humo.
Miongoni
mwa mastaa hao ni Martin Kadinda ambaye hata hivyo uwepo wake Visiwani
Unguja ulizua na kuezua maswali mengi, kwani licha ya kuonekana pekee
yake, ilidaiwa kuwa alikuwa na Wema Sepetu, ambaye alibaki hoteli.
Mastaa
wengine ni msanii wa hip hop, Farid Kubanda ‘Fid Q’, star wa tamthilia
ya Siri ya Mtungi, Juma Rajab ‘Cheche’ ama Zoba na wengine.
Mahaba niuwe….!
Bata likiendelea kwenye fukwa za visiwani Zanzibar.
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon