جاءت امرأة الى النبي صلى الله عليه والسلام فقالت : يا رسول الله إن لي ابنة عريسا أصابها حصبة فتمرق )تساقط( شعرها أفأصله ؟ فقال : لعن الله الواصلة والمستوصلة "
" Alikuja Mwanamke mmoja kwa Mtume Akasema: Ewe Mjumbe wa mwenyezi mungu Mimi nina binti yangu bi harusi amepatwa na surua na nywele zake zinaanguka.je niziunganishe ( kwa nywele za bandia ) akasema Mtume :
" Amemlaani Mwenyezi mungu mwenye kuunganisha nywele na mwenye kutaka kuunganishiwa ."
Ameipokea Musilimu 3/ 1676.
Na imepokewa kutoka kwa jaabir bin Abdillah Akisema :
زجر النبي صلى الله عليه وسلم أن تصل المرأة برأسها ....
" Mtume Amekataza kwa mwanamke kuunganisha chochote kwenye kichwa chake . "
Ameipokea Musilimu 1679.
Na mfano wa hii ni hizi nywele za bandia zinazojulikana kwenye zama zetu kwa jina la ( wigi ) au baroka . Na wenye kuunganisha nywele kwenye zama zetu ni hawa watu wa saloon.
Na mfano wa haramu hii vile vile kuvaa nywele za kuazima kama wanavyofanya baadhi ya waigizaji wa kike na kiume wasiokuwa na tabia nzuri kwenye tamthilia na michezo ya kuigiza .
اللهم اشهد ان لا اله الا انت استغفرك واتوب اليك.
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon