Wakati
wa kufungua mwaka, mfalme wa taarab Mzee Yussuf akaamua kubadili
usafiri wake kwa kuachana na Toyota Ipsum na kununua Toyota Harrier
(pichani juu) yenye thamani ya milioni 35.
Gari
hilo bab kubwa likaingia kwenye mitandao ya kijamii, wengi wakimpongeza
Mzee Yussuf huku wachache wakimpiga vijembe kwa madai ya kuwa yeye siyo
msanii wa kwanza wa taarab kumiliki usafiri wa bei mbaya. Akatajwa
Zuhura Shaaban mwenye kumiliki Hummer.
Lakini
Mzee Yussuf ameiambia Saluti5 kuwa anayachukulia maneno hayo kama mambo
ya kawaida kutoka kwa walimwengu na kwamba hafanyi maisha yake kwaajili
ya kushindana na mtu bali ni kwa manufaa yake na familia yake.
“Nimekuwa
nikibadili usafiri mara kwa mara, namshukuru Mungu kwa kuniwezesha
kupata gari la ndoto yangu, sijui kesho au kesho kutwa panapo majaaliwa
nitatamani au nitamiliki gari gani, Mungu ndo anajua,” alisema Mzee
Yussuf.
“Haya
ni maisha ya kawaida, kila mtu ana njozi zake na mipango yake, sifanyi
kitu kwa kushindana na mtu bali natii kiu yangu,” aliongeza Mzee Yussuf.
Hata
hivyo wakati watu wakiitolea macho Harrier ya Mzee Yussuf, Saluti5
imebaini kuwa msanii huyo anamiliki malori mawili (tipa) aina ya Scania
ambayo yako Chanika yakifanya kazi kwenye kampuni yake ya uuzaji na
usambazaji wa vifaa vya ujenzi.
Ni gari za bei mbaya - ukizilinganisha thamani yake na Toyota Harrier ni sawa na kichuguu na mlima. Huyo ndo Mfalme Mzee Yussuf.
Gari la Mzee Yussuf linavyoonekana kwa ndani
Gari la Mzee Yussuf linavyoonekana kwa nje
Sehemu ya ndani ya gari hilo upande wa mbele
Kitu kimetulia
Likiwa limebaki mbele ya ofisi za Saluti5 Kinondoni jijini Dar es Salaam
Hakika ni gari la starehe
Mzee Yussuf akiwa ametulia ndani ya mchuma wake
Moja ya Scania anazozimiliki Mzee Yussuf
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon