Jibu: Suala
hilo linadhibitiwa kupitia vikao vya serikali za mtaa kwa kuwa ndiyo
wanajadili na kupitisha hayo hivyo wananchi washiriki mikutano ya
serikali za mitaa na kuhoji hayo. Mikutano hiyo huitishwa kila baada ya
miezi miwili hivyo wananchi wahudhurie kwa kuwa wengi hawahudhurii.
2. Yusuph Abdalah mkazi wa Darajani
Ni lini daraja la JKT njia panda ya Coca Cola Kawe litajengwa kwa kiwango cha zege ili kulifanya liwe imara?
Jibu: Kiujumla
katika halmashauri ya Kinondoni tumekuta kuna changamoto nyingi za
utekelezaji wa miradi ya maendeleo na hiyo ni kutokana na makusanyo
madogo ya Sh8 bilioni walizokuwa wanakusanya zamani kabla ya kuingia
sisi. Katika fedha hizo walikuwa wanatenga Sh1 bilioni kwa ajili ya
maendeleo na pale kuna majimbo matatu Kawe, Kinondoni na Ubungo. Hivi
sasa tumefanikiwa kufikisha makusanyo ya Sh37 bilioni na kati ya hizo
Sh13 bilioni ni za miradi ya maendeleo. Tumejenga barabara za lami mpya
nne katika eneo la Mikocheni Tumejenga daraja kubwa la Nyerere.
Changamoto ya hilo la njia panda tutalifanyia kazi katika mwaka huu wa
fedha 2015/16, lakini kinachotakiwa kufanyika ni wananchi kuhakikisha
mwenyekiti wa mtaa wa Mikocheni B kupeleka kwa WDC ili ipitie na
kuileta kwenye vikao vya halmashauri ambavyo mimi naingia ili tuweze
kulishughulikia.
3. Godlove Jophrey mkazi wa Kawe.
Mimi
ni miongoni mwa wananchi wengi wanaoishi Kawe ambao tulipanda mbegu
DEC, lakini mambo yaliyojitokeza yametufanya wengi wetu tusijue hatima
ya fedha zetu hadi leo, hivyo tumeyumba kiuchumi. Utatusaidia vipi kujua
hatma ya fedha zetu?
Jibu: Suala
la DEC tumelizungumzia na hivi sasa lipo mikononi mwa Serikali.
Tumeomba Serikali irudishe fedha hizo kwa wananchi na sisi kama
watumishi tuna mipaka yetu na hapo ndipo tulipofikia kwamba Serikali
ndiyo inapaswa kuzirudisha hizo fedha kwa wananchi.
4. Gaudence Manyanga mkazi Mzimuni.
Kawe
Mzimuni na Ukwamani hakuna sehemu ya kutupia taka hivyo kumekuwa na
hali ya utupaji ovyo wa taka ambao unachafua mazingira na kuhatarisha
afya za wakazi wa maeneo hayo, unatusaidiaje kupata eneo maalumu la
kutupa taka?
Jibu: Eneo
la kutupa taka ni miongoni mwa mambo ambayo tayari tumelifanyia kazi,
tumeshakaa na watendaji na wenyeviti wa serikali za mitaa kutafuta eneo
maalumu la kutupa taka kwa eneo la Ukwamani na Mzimuni.
Endelea Kuisoma Habari hii hapa>> http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/MASWALI-10-KWA-MBUNGE-WANGU--Halima-Mdee/-/1597296/2626424/-/vje7no/-/index.html
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon