Msanii wa muziki wa asili, Mrisho Mpoto ameanza kushoot video ya wimbo
wake mpya ‘Njoo Uichukue’ ndani ya uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam
pamoja na sehemu nyingine.

Mpoto akiimba
Mpoto akiimba
Akizungumza na Bongo5 leo msemaji wa Mpoto Theatre Gallery Ltd , Dominic
Kaunda, alisema ndani ya video hiyo inayofanyWa na director Adam Juma
wamewatumia Kitale na Stan Bakora ili waigize kama ni wazee wa uswazi.
“Tunashukuru mungu kazi imeenda poa, tumemaliza kushoot video na Adam
juma na baada ya kama wiki moja itatoka,” amesema. “Tumetumia gharama
kubwa kidogo kwa sababu tumekodi uwanja wa taifa kutwa nzima, tumewalipa
wale jamaa wa mkude simba, irector Adam Juma pamoja watu ambao
wataonekana kwenye hiyo video. Kwahiyo ni gharama kubwa kidogo sema
siwezi itaja kwa sasa kwa sababu hivi ni vitu vya ndani ya kampuni.
Tumejifunza sasa kuacha kuropoka kuhusu gharama tulizotumia tunataka
watu waangalie ubora wa kazi.”
Mpoto akiwa mtaani katika hatua za kushoot video
Mpoto akiwa na Adam Juma ndani ya uwanja wa taifa
Mpoto, Kitale, Stan Bakora
Mpoto
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon