Real
Madrid waliingiza mguu mmoja kwenye hatua ya robo fainali ya ligi ya
mabingwa wa ulaya jana usiku baada ya kupata ushindi wa magoli mawili
kwa bila dhidi ya Schalke 04 mjini Gelsenkirchen.
Usiku wa jana pia, Cristiano Ronaldo na wenzie waliweza kuendelea kuvunja na kuweka rekodi mpya katika michuano hii.
Hapa, najaribu kukueletea takwimu mbalimbali za rekodi walizoweka Madrid na Ronaldo baada ya mchezo wa jana.
76 – Ronaldo sasa ametimiza jumla ya magoli 76 na kuwafikia Lionel Messi na Raul katika michuano yote ya ulaya.
72 –
Nahodha huyo wa Ureno anahausika zaidi ya robo ya magoli yote
yaliyofungwa na wareno kwenye ligi ya mabingwa wa ulaya – magoli 72 kati
ya 274.
58 – Goli la Ronaldo jana usiku lilikuwa goli la 58 katika Champions League – akiwa amevalia jezi za Real Madrid.
29 –
Mpaka kufikia usiku wa jana Ronaldo anaongoza kwa magoli na assists kwa
misimu miwili katika michuano hiyo ya ulaya. Ukiunganisha magoli na
assists Ronaldo anaongoza kwa umbali mrefu – akiwa na jumla ya magoli +
assists 29 – huku anayemfuatia Lionel Messi akiwa na 18.
28 –
Ushindi wa jana usiku umemfanya Ronaldo atimize idadi ya ushindi katika
mechi 28 za champions league, na kwa kufanya hvyo sasa amewapita Edwin
van der Sar na Victor Valdes waliokuwa wakiongoza.
12 – Goli lake la kichwa jana lilikuwa la 12 mfululizo kwa Ronaldo kufunga ugenini katika michuano ya ulaya.
10 – Ushindi wa 2-0 dhidi ya vijana wa Roberto di Matteo umeifanya Madrid kushinda mara 10 mfululizo katika Champions League.
6 –
Ronaldo ni mchezaji pekee wa sita kuweza kufunga magoli 10 au zaidi ya
kichwa katika michuano ya ulaya. Anaungana na Fernando Morientes, Raul,
Inzaghi, Jardel na Andriy Shevchenko katika listi hiyoSign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon