“Kama wao wameweza kutufunga mabao mawili kwao
kwanini sisi tushindwe kuwafunga kwetu? Beki yao pia nimeona siyo nzuri
sana, kama tukicheza kwa kushambulia tunaweza kupata mabao mengi.
BDF ilifungwa mabao 2-0 na Yanga katika mechi ya
kwanza ya Kombe la Shirikisho barani Afrika mchezo uliochezwa Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam juzi Jumamosi. Zitarudiana mbili zijazo huko
Botswana.
Nzombe alisema Yanga iliweza kuwafunga mabao hayo
kwa kutumia vizuri faida ya uwanja wa nyumbani jambo ambalo
haliwakatishi tamaa kwani nao wanaweza kufanya hivyo watakapokutana
katika mechi marudiano nyumbani kwao.
“Kwanza sikutarajia kama Yanga inacheza soka kiasi
kile, nilidhani ni timu ya kawaida lakini kiwango walichokionyesha
kimenishangaza kidogo, inabidi kujipanga kwa ajili ya mechi ya
marudiano,” alisema.
“Kama wao wameweza kutufunga mabao mawili kwao
kwanini sisi tushindwe kuwafunga kwetu? Beki yao pia nimeona siyo nzuri
sana, kama tukicheza kwa kushambulia tunaweza kupata mabao mengi.
“Yule namba 27 (Simon Msuva) na kiungo wao mmoja
wamecheza vizuri sana, walikuwa sumu kwa mabeki wetu na ninaweza kusema
ndiyo wachezaji waliofanya vizuri zaidi kwa upande wa Yanga.
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon