Kocha wa Yanga, Hans Pluijm alisema:
“Walikuwa wengi nyuma katika mchezo wa Dar es Salaam, ilikuwa ngumu
kuwafanya wafunguke ili tuweze kupita, tulichofanya mpaka tukawafunga
zipo klabu nyingi Ulaya kinawashinda, lakini najua sasa nini tufanye
tukiwa kwao.
BENCHI la Ufundi la Yanga limewashtukia BDF XI
ya Botswana kwamba hawakucheza katika ubora wao, hivyo limemtanguliza
haraka mtaalamu nchini humo ambaye atafanya ushushushu wa haraka na
kukamilisha mipango yote.
Akizungumza na Mwanaspoti, Katibu Mkuu wa Yanga,
Dk Jonas Tibohora, ambaye ana uelewa mkubwa wa masuala ya ukocha na
ufundi, alisema benchi la ufundi la timu yao limemuagiza aondoke leo
kuifuata timu hiyo kuwasoma watakapokuwa wakicheza mchezo wa LigiKuu
Botswana kabla ya kurudiana na Yanga.
BDF XI ambayo juzi Jumamosi ilikubali kipigo cha
mabao 2-0 katika mchezo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho, keshokutwa
Jumatano itashuka katika Uwanja wa SSKB kucheza na Orapa United katika
ligi ya kwao.
Alisema mbali na jukumu hilo, pia atakuwa na kazi
ya kufuatilia kila kitu kuhusu sehemu itakapofikia kikosi chao kwa
mchezo wa marudiano.
“Kocha wetu ameona hilo kwamba kuna haja ya
kumtuma mtu kutangulia huko na wakaona mimi niende nikafanye hiyo kazi
ili niwape ripoti, tulitaka tumuagize Mkwasa (Charles) lakini kutokana
na hizi mechi mbili za ligi tumeona abaki aongeze nguvu,” alisema
Tibohora kuhusiana na kocha msaidizi huyo
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon