Sign up here with your email
WALIOWAJERUHI POLISI TZ WASAKWA
Polisi nchini Tanzania
Polisi nchini Tanzania wamesema wanawasaka watuhumiwa waliowajeruhi askari
sita kwa risasi mkoani Tanga.
Askari hao walijeruhiwa wakati wakifanya kazi ya kuwatafuta watuhumiwa wa
uhalifu wa kutumia silaha wanaodaiwa kuwa walijificha eneo moja nje ya mji
wa Tanga wakiwa na silaha.
Awali kulizagaa taarifa na hofu kuwa wahusika walikuwa na itikadi za
kigaidi, lakini taarifa ya maandishi iliyotolewa na polisi imewaita watu
hao kuwa ni majambazi na kwamba msako wa kuwatafuta unaendelea
ConversionConversion EmoticonEmoticon