Timu ya Stand United ya mjini
Shinyanga imeinyuka club ya Simba bao moja kwa nunge katika mchezo wa ligi kuu
ya Vodacom Tanzania Bara mchezo ulipopigwa jioni hii katika uwanja wa CCM
Kambarage mjini Shinyanga.
Goli la Stand United (Chama la
Wana) limefungwa na Abasirim Chidiebele kipindi cha kwanza
mapema dakika ya 10 alifunga bao la kichwa kilichomshinda golikipa namba
moja wa timu ya Simba Ivo Mapunda na kutinga moja kwa moja katika nyavu za goli
la timu hiyo.
Katika mchezo huo ulioshuhudiwa
na maelfu ya wapenzi wa soka kutoka Shinyanga na nje ya Shinyanga ulijawa na
vituko vingi ambapo kabla ya mchezo huo shabiki mmoja wa timu ya Simba
aliyefahamika kwa jina la Rajabu Jota alikamatwa na mashabiki wa Stand
United akimwaga dawa katika mlango wa kutokea wachezaji wa timu ya Stand
United.
Kitendo hicho kilisababisha
mashabiki wa Stand kumchapa makofi na makonde kabla ya jeshi la polisi kufika
eneo la tukio na kumchukua mtuhumiwa.
Baada ya mchezo kuisha kocha
mkuu wa timu ya Stand Mathias Lure ameeleza kufurahishwa na matokeo hayo na
kuahidi kuwa ataendelea kufanya mabo makubwa katika timu yake.
Kwa upande wake kocha mkuu wa
Simba Golan Kuponovic amesema Stand siyo timu ya kubeza ni timu nzuri ndiyo
maana wameshinda katika mchezo huo.
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon