DRFA,YAMLILIA KIUNGO WA ZAMANI WASIMBA NA TAIFA STARS-CHRISTOPHER ALEX

Chama chakandanda mkoa wa Dar es salaam DRFA,kimeeleza kusikitishwa kwake na kifo
chamchezaji kiungo wa zamani wa klabu ya simba na timu ya
taifa-TaifaStars,Christopher Alex  maarufu kama Masawe,kilichotokealeo (februari 22
mwaka huu),katika Hospitali ya Mirembe Dodoma.
Mwenyekiti waDRFA,Almas Kasongo,amemuelezea marehemu Christopher kuwa ni mchezaji
aliyevumaenzi za uhai wake na kuiletea heshima kubwa klabu yake ya Simba na Taifa
Kwaujumla,pale walipofanikiwa kuisukumiza nje ya michuano ya afrika klabu ya
Zamalekna kuivua ubingwa miamba hiyo ya soka ya kaskazini mwaka 2003.
Kiungo huyoaliyeanza kuvuma katika miaka ya 2000,amefariki dunia kutokana na
kusumbuliwakwa muda mrefu na ugonjwa wa kifua kikuu (TB).
Marehemu ChristopherAlex, alizaliwa Septemba 12 mwaka 1975,na kupata elimu yake ya
msingi katikashule ya msingi Uhuru na kumaliza katika shule ya Chamwino huko Dodoma
mwaka1993,na alianza kucheza mpira kwenye timu ya Daraja la nne Chamwino UTD
nabaadaye daraja la tatu akiwa na kikosi cha Aston Villa nayo ya Dodoma.

Mwaka 1999-2001ameitumikia klabu ya CDA ya Dodoma,kabla ya kutimkia klabu ya Reli
mwaka 2002na baadaye kujiunga na wekundu wa msimbazi Simba,Marehemu ameacha mtoto
mmoja aitwayeAlex.

Kasongo,kwaniaba ya kamati ya utendaji ya DRFA,wametoa ubani wa shilingi laki
mbili(200,000/=) kwa familia ya marehemu,na kuwataka mashabiki wa soka na
watanzaniakwa ujumla kuungana pamoja katika kuifariji familia hiyo kwenye kipindi
hikikigumu cha majonzi.

Previous
Next Post »