Yanga SC kwenda Botswana Alhamisi

Kikosi cha timu ya Yanga kitaondoka nchini Alhamisi ijayo kuelekea Botswana kwa ajili ya mechi yao ya marudiano ya hatua ya awali ya Ligi ya kombe la Shirikisho Afrika. Yanga ilishinda 2-0 katika mechi yao ya kwanza kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Jumamosi.  
 
Akizungumza na NIPASHE jana, Katibu Mkuu wa Yanga, Dk. Jonas Tiboroha, alisema kikosi hicho kitaondoka jijini kikiwa na wachezaji wote watakaokuwa wazima.
 
Alisema kwa sasa wachezaji wote wako imara na tayari wapo jijini Mbeya kwa ajili ya kujiandaa na mechi yao ya kesho dhidi ya Prisons ya huko na ya Jumapili dhidi ya Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine.
 
Alisema tayari maandalizi mazito yanaendelea kuhakikisha kwamba wanashinda mechi yao ya marudiano dhidi ya BDF XI na kutinga katika hatua ya kwanza.
 
CHANZO: NIPASHE
Previous
Next Post »