Msuva amefikisha magoli 6 mawili nyuma ya Didier Kavumbagu wa Azam fc
Na Mwandishi Wetu, Mbeya
YANGA SC
imeitungua Tanzania Prisons mabao 3-0 katika mechi ya ligi kuu soka
Tanzania bara iliyomalizika jioni hii uwanja wa CCM Sokoine, Mbeya.
Mabao ya Yanga yamefungwa na Saimon Msuva (dakika ya 3, 62’ na Andrey Coutinho 11’).
Kwa
matokeo hayo, Yanga wameishusha Azam kileleni baada ya kufikisha pointi
28 katika mechi 14 walizocheza na wanawaacha Azam nafasi ya pili wakiwa
na pointi 26 kwa mechi 14 walizocheza baada ya jioni hii kutoka suluhu
(0-0) na Ruvu Shootings uwanja wa mabatini, Pwani.
Licha ya kuwazidi Azam kwa pointi, Yanga pia wamewazidi wanalambalamba wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Azam
wamefunga magoli 22 na kufungwa 12, tofauti ya magoli ya kufunga na
kufungwa ni 10, wakati Yanga wao wamefunga magoli 18 na kufungwa 7,
tofauti ni 11.
Ushindi wa leo ni salamu tosha kwa Mbeya City fc ambao watachuana na Yanga katika uwanja wa Sokoine, jumapili ya wiki hii.
Tanzania Prisons wameendelea kuburuza mkia wakijikusanyia pointi 11 tu katika mechi 14 walizoshuka dimbani.
Coutinho
REPOTI YA MECHI
Mapema
dakika ya 3’ Simon Happygod Msuva aliifungia Yanga bao la kuongoza
akimalizia mpira wa kona uliochongwa na kiungo mshambuliaji raia wa
Brazil, Andrey Coutinho.
Msuva aliruka juu sambamba na kipa na mpira ulipotua aliugusa kwa mbali na ukamponyoka mlinda mlango na kuzama goli.
Wachezaji wa Prisons walihamaki wakiamini Msuva amemsukuma kipa, lakini mwamuzi akahesabu bao.
Bao la
pili lilifungwa dakika ya 11’ ya kipindi cha kwanza ambapo Coutinho
alipiga shuti la kawaida, beki wa Prisons akiwa katika harakati za
kuokoa alijifunga mwenyewe.
Yanga
waliendelea kucheza vizuri, wakigongeana pasi na kufika eneo la hatari
la Prisons, lakini safu ya Prisons ilifanya vizuri licha ya kupata
misukosuko.
Katika kipindi hicho, Prisons walitulia baada ya kufungwa na kupata nafasi kadhaa, lakini walishindwa kuzitumia.
Mpaka dakika 45’ za kipindi cha kwanza zinamalizika, Yanga walikuwa mbele kwa mabao 2-0.
Kipindi
cha pili, Prisons walianza kutafuta mabao ya kuzawazisha, lakini Yanga
waliendelea kuonesha uzoefu wao wakiwatuliza vizuri.
Katika dakika ya 62’ Andrey Coutinho aliingiza kona maridadi na Msuva akapiga kichwa ‘ndosi’ na kuzamisha goli la tatu.
Msuva
alipata upenyo huo kutokana na uzembe wa beki wa Prisons, Salum Kimenya
aliyekuwa anamuangalia tu wakati akimtoka kupiga kichwa.
Coutinho leo hii amefunga goli na kusababisha magoli mawili ya Msuva kutokana na mipira yake ya kona.
Msuva
amefikisha mabao 6 msimu huu, magoli mawili nyuma ya kinara wa kupachika
mabao, mshambuliaji wa Azam fc, Didier Fortune Kavumbagu.
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon