Na Makongoro Oging’
JESHI la Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni jijini Dar, linamsaka mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Godfrey Mushi kwa kosa la kumshambulia na kumjeruhi Robert Ridoch Tillya ambaye ni mfanyakakazi wa Kampuni ya Global Publishers Limited.
Mushi ambaye awali alijitambulisha kwa Tillya kama ni askari polisi anadaiwa kufanya kosa hilo Februari 15, mwaka huu saa 11.45 alfajiri karibu eneo la Bamaga Mwenge.Tukio hilo limeripotiwa katika Kituo cha Polisi Kijitonyama na kufungua kesi yenye jalada namba KJN/RB/1941/2015 Shambulio la Mwili.
Akizungumzia tukio hilo, Tillya alisema lilimtokea alfajiri mara tu baada ya kuegesha gari ofisini kwao na yeye kwenda kituo cha daladala ili apande gari kurejea nyumbani kwake kwa mapumziko. Alisema alimuona kijana mmoja akija upande wake akikimbia, lakini muda mfupi baadaye akafika Mushi na kumtaka amuonyeshe alikokimbilia mtu huyo, akidai walikuwa wote, jambo ambalo halikuwa kweli kwani alikuwa hamfahamu.
“Nilijitetea na kumjibu kuwa simjui, alijitambulisha kuwa yeye ni polisi, nami nilimwonyesha kitambulisho changu cha kazi na kumtaka twende hadi ofisini kwetu wakamuulize mlinzi kama sikutoka huko, alikataa, akawa ananipiga.
“Pembeni kulikuwa na gari jeusi aina ya Noah yenye namba za usajili T 860 BYG, alinichukuwa na kuniingiza mle, walinipiga na kunizungusha sehemu mbalimba baadaye walianichia nikiwa hoi nikaenda hospitali,” alisema Robert.
Afisa mmoja wa polisi Mkoa wa Kinondoni idara ya upelelezi ambaye alisema yeye siyo msemaji alikiri kuwa na taarifa ya tukio hilo na akasema wanafanyia uchunguzi. Picha iliyotumika ukurasa wa nyuma ilipatikana kwenye simu ambayo watekaji waliitumia siku ya utekaji na ikapatikana kwenye Mtandao wa WhatsApp.
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon