Kiungo wa timu ya Coastal Union, Godfrey Wambura wa kwanza kulia akiwa katika moja ya mechi za ligi kuu tanzania bara msimu huu
Kiungo wa timu ya Coastal Union, Godfrey Wambura wa kwanza kulia akiwa katika moja ya mechi za ligi kuu tanzania bara msimu huu
Kiungo wa timu ya Coastal Union, Godfrey Wamb ura
amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Februari 2015 wa Ligi Kuu ya
Vodacom (VPL) nayoendelea kutimua vumbi kwenye viwanja mbalimbali
nchini.
Wambura
amechaguliwa kuwa mchezaji bora baada ya jopo la makocha linalofanya
majumuisho ya wachezaji bora wa kila mchezo, ambapo kiungo huyo ameweza
kuwapiku wachezaji Saimon Msuva wa Young Africans, Abasirim Chidiebere
wa Stand United na Gideon Benson wa Ndanda FC.
Kwa
kuibuka mchezaji bora wa mwezi Februari, Wambura atazawadiwa fedha
taslimu sh. milioni moja kutoka kwa wadhamini wa ligi hiyo kampuni ya
simu za mkononi ya Vodacom.
Jopo
maalumu la makocha waliopo katika viwanja vyote vinavyotumika kwa mechi
za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) ndiyo wanaofanya kazi ya kuchagua mchezaji
bora kwa kila mechi kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa, na baadaye
alama zao kujumlishwa ili kumpata mshindi wa mwezi.
Wakati
huo huo timu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars) inatarajiwa kuagwa
mbele ya waandishi wa habari kesho alhamisi saa 5 kamili katika ukumbi
wa TFF Karume.
NB: Ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom (imeambatanishwa)
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon