
Kanisa la Presbyterian nchini Marekani ambalo lina takriban wanachama 
millioni 2 ,limebadilisha sheria yake ya ndoa na kuwajumuisha watu wa 
jinsia moja.
Kanisa hilo ambalo linashirikisha idadi kubwa ya wanachama wake duniani 
lilitoa tangazo hilo baada ya idadi kubwa ya magavana wa majimbo yake 
171 kuidhinisha mabadiliko hayo.
Sheria yake mpya sasa itasoma kwamba ndoa ni makubaliano ya kipekee kati
 ya watu wawili ikilinganishwa na makubaliano kati ya mume na mke.
Sheria hiyo ilioidhinishwa na baraza kuu la kanisa hilo mwaka uliopita ilikubaliwa na zaidi ya nusu ya majimbo ya kanisa hilo.
Mkutano wa makundi katika jimbo la New Jersy ulikuwa wa 86 kuidhinisha sheria hiyo.
Uamuzi huo unatarajiwa kuzua mgawanyiko mkubwa kati ya wanachama wa kanisa hilo ambao wanapinga sheria hiyo.
Mwaka uliopita baraza kuu la kanisa hilo lilitoa idhini kwa wachungaji 
wake kuwafungisha ndoa wapenzi wa jinsia moja katika majimbo ambayo ndoa
 hizo zinaruhusiwa.
Sign up here with your email
 
ConversionConversion EmoticonEmoticon