MAPENZI YALINIUA NA BUSARA ZIKANIPONZA LEO HII NIPO HIVIII



SINTASAHAU HAYA

Miaka 10 ya ndoa yetu siku moja niliingia
nyumbani nikamkuta mke wangu akiniandalia
chakula cha usiku. Nilimshika mkono na
kumwambia: Nina jambo ninalotaka
kukueleza.Alikaa na kunisikiliza kwa makini.
Dalili za wasiwasi nilikuwa nikizishuhudia
machoni mwake. Ghafla nilijikuta katika hali ya
kushindwa
kukifungua kinywa changu. Lakini ilikuwa ni
lazima ajue ninachokifikiria, hivyo nilipiga
moyo
konde, nikamwambia kwa upole: Ninataka
tuachane.Hakuonekana kuudhika kwa hoja
niliyokuwa nimeiwasilisha mbele yake, bali
aliniuliza kwa sauti ya upole kabisa: Kwa
nini? Nilijaribu kulikwepa hilo swali, hivyo
alighadhibika sana na kuniambia kwa sauti ya
juu: Wewe si mwanaume! Usiku ule
hatukusemeshana, na muda wote alikuwa
akilia. Nilitambua kuwa alitaka kujua kitu gani
kimetokea katika ndoa yetu. Lakini sikuweza
kumpa jibu lenye kuridhisha; kwa sababu
sikuwa na mapenzi naye tena, moyo wangu
ulikuwa umetekwa na binti mwingine aitwaye
Jane. Nilimsikitikia sana! Huku nikiwa na hisia
za hatia moyoni mwangu,
niliandika pendekezo la talaka ambalo lilieleza
kuwa atachukua nyumba yetu, gari na shea ya
asilimia 30 ya kampuni yangu. Mke wangu
aliitazama karatasi hiyo kisha akaichana na
kuitupa kwenye ndoo ya takataka. Huyu ni
mwanamke aliyekuwa ameishi nami kwa
muda
wa miaka kumi alikuwa amegeuka kuwa kama
mgeni kwangu. Nilisikitika sana na kumuomba
radhi kwa kumpotezea muda, rasilimali na
nguvu zake lakini sikuweza kutengua kauli
yangu kwa sababu nilikuwa nikimpenda sana
Jane na nilikuwa nimezama kweli kweli ndani
ya
huba lake na kuwa teja wa penzi lake.
Hatimaye
alilia kwa sauti mbele yangu, jambo ambalo
nilikuwa nikitarajia kuliona. Kilio chake kwangu
kilikuwa kama faraja. Wazo la talaka
lililonitawala kwa wiki kadhaa lilikuwa likizidi
kupata nguvu na sasa lilionekana kuwa wazi
kabisa. Siku iliyofuata nilirudi nyumbani nikiwa
nimechelewa na kumkuta akiandika kiandika
kitu mezani. Sikutaka kula chochote zaidi ya
kuelekea moja kwa moja kitandani kwa
sababu
nilikuwa nimechoka sana kutokana na
mishemishe za siku hiyo nikiwa na Jane.
Niliposhtuka, bado alikuwa hajatoka mezani.
Sikujali hata kidogo, nikageuka na kuendelea
kuuchapa usingizi. Asubuhi alinipatia masharti
ya talaka: hakutaka
mali yoyote kutoka kwangu, bali alitaka kuwe
na muhula wa mwezi mmoja kabla ya talaka.
Alitaka kwamba katika kipindi hicho tujaribu
kuishi kama kawaida kwa kadiri iwezekanavyo.
Hoja yake ilikuwa wazi: mtoto wetu alitarajia
kufanya mitihani ya shule ndani ya mwezi huo
na hakutaka tumchanganye kwa tukio la
talaka. Hili nililikubali. Lakini alikuwa na
nyongeza:
alinitaka nikumbuke siku ya ndoa yetu
nilipomnyanyua kumpeleka chumbani kwetu.
Alitaka kwamba katika kipindi hicho cha mwezi
mzima niwe nambeba kila siku asubuhi
kumtoa

chumbani mpaka mbele ya mlango wa nje ya
nyumba. Nilihisi kuwa alikuwa ameshikwa na
wendawazimu. Nilikubali ombi lake kwa
sababu
niliona kuwa mwezi mmoja sio kitu, kwani
nilitaka tuachane. Nilimsimulia Jane kuhusu
masharti ya talaka
yaliyotolewa na mke wangu. Alicheka sana na
kuona kuwa ni upuuzi. Hata akitumia hila gani
lazima apewe talaka,alisema Jane kwa
masihara. Tangu nilipoelezea nia yangu ya
kutaka kuachana naye, hatukuwa na uhusiano
wa kimwili na mke wangu. Hivyo nilipombeba
siku ya kwanza, sote tulionekana kutokuwa na
uchangamfu. Mtoto wetu alifurahi na kupiga
makofi: Baba amembeba mama. Kauli yake
ilinipa maumivu moyoni. Kutoka chumbani
mpaka barazani, kisha mlangoni, nilitembea
mita kumi nikiwa nimembeba mikononi
mwangu. Aliyafumba macho yake na
kuniambia
kwa upole na ulaini: Usimwambie mtoto wetu
kama tunaachana.Nilikubali kwa kutikisha
kichwa huku nikiwa

nimefadhaika. Nilipofika nje nilimshusha
akaenda kituoni kusubiri basi, nami
nikachukua
gari langu na kwenda ofisini nikiwa peke
yangu. Siku ya pili tulijaribu kutoonesha hali
yoyote ya
mifarakano. Aliegemea kifuani kwangu nikahisi
manukato mazuri ya blauzi yake. Nilibaini
kuwa
sikuwa nimemtazama vizuri mke wangu kwa
muda mrefu. Uso wake ulikuwa umeanza
kuwa
na mikunjo na nywele zake zilikuwa zimeanza
kubadilika. Ndoa yetu ilikuwa imemfanya
achoke.

 Siku ya pili tulijaribu kutoonesha hali
yoyote ya
mifarakano. Aliegemea kifuani kwangu nikahisi
manukato mazuri ya blauzi yake. Nilibaini
kuwa
sikuwa nimemtazama vizuri mke wangu kwa
muda mrefu. Uso wake ulikuwa umeanza
kuwa
na mikunjo na nywele zake zilikuwa zimeanza
kubadilika. Ndoa yetu ilikuwa imemfanya
achoke. Kwa dakika kadhaa niliduwaa na
kuwaza kile nilichokuwa nimemfanyia. Siku ya
nne nilipombeba nilihisi aina ya ukaribu
na mvuto ikirejea. Huyu ni mwanamke
aliyekuwa amenipa miaka kumi ya uhai na
maisha yake. Siku ya tano na ya sita, kwa
mara nyingine,
niliona hali ya ukaribu na mvuto fulani ikirejea
kati yetu. Sikumsimulia Jane kuhusu hali hii.
Kadiri siku zilivyosonga mbele ndivyo
nilivyozidi
wepesi wa kumbeba. Yumkini ilisababishwa na
ile hali ya kumbeba kila siku kiasi cha
kumuona kuwa ni mwepesi. Asubuhi moja
alikuwa akichagua nguo ya
kuvaa. Alijaribu nguo kadhaa lakini hakupata
inayomfaa. Alishusha pumzi na kusema: Nguo
zangu zote hazinienei, zimekuwa kubwa.
Nilibaini kuwa alikuwa amekonda na ndiyo
maana niliweza kumbeba kwa urahisi.
Nilisikitika kwa sababu nilihisi kuwa alikuwa
amebeba mambo mengi moyoni mwake. Hivyo
nilimsogelea na kukipapasa kichwa chake. Ni
wakati huo ambapo mtoto wetu aliingia na
kusema: Baba sasa ni muda wa kumbeba
mama. Tukio la kumuona baba yake akiwa
amembeba mama yake lilimuathiri na kuwa
sehemu muhimu sana ya maisha yake. Mke
wangu alimuita na kumkumbatia kwa upendo.
Niligeuza uso wangu pembeni, sikutaka
kuangalia tukio hilo nisinje nikabadilisha
uamuzi wangu wa talaka. Nilimnyanyua na
kumbeba mke wangu, nikatembea kutoka
chumbani, sebuleni mpaka nje. Aliizungusha
mikono yake mizuri shingoni kwangu, nami
nikamshikilia vizuri; ilikuwa kana kwamba ni
siku ile ya harusi yetu. Lakini wepesi wa mwili
wake ulinifanya niwe mwenye huzuni. Siku ya
mwisho nilipombeba niliingiwa na uzito
wa kupiga hatua. Wakati huo mtoto wetu
tayari
alikuwa shule. Nilimshikilia vizuri na kusema:
Sikuwa nimejua kuwa maisha yetu yamekosa
mvuto. Niliwasha gari kuelekea ofisini,
niliamua kupita kwa Jane. Nilipofika nilitoka
haraka bila hata kuubana mlango wa gari.
Nilikuwa na wasiwasi nisije nikaghairi nia
yangunikapandisha ngazi. Jane alipofungua
mlango nilimwambia: Samahani Jane, sitaki
kuachana na mke wangu. Alinitazama kwa
mshtuko na kunigusa kwenye
paji la uso. Una homa? alisema. Niliutoa
mkono wake na kumwambia: Samahani Jane,
sitaki kumuacha mke wangu. Yawezekana
maisha yangu na mke wangu yalikosa
uchangamfu kwa sababu hatukuwa karibu, sio
kwa sababu hatukupendana. Sasa nimebaini
kwamba kwa kuwa nilimbeba siku ya ndoa
yetu,
ninapaswa kuendelea kufanya hivyo mpaka
kifo
kitutengenishe.Jane alionekana kushtuka
sana. Alinizaba kibao, akaubamiza mlango na
kuanza kulia. Nilimuacha nikapanda gari na
kuondoka. Njiani
nilipita kwenye duka la maua nikaagiza shada
la
maua kwa ajili ya mke wangu. Muuzaji
akaniuliza ujumbe unaotakiwa kuandikwa juu
ya kadi nikatabasamu na kumwambia aandike:
Kila siku asubuhi nitakubeba mpaka kifo
kitakapotutenganisha. Jioni nilifika nyumbani
nikiwa na maua
mkononi, tabasamu usoni, nikapandisha
mpaka ndani. Nilipofika chumbani mke wangu
alikuwa amelala akiwa amefariki dunia. Kumbe
alikuwa akipambana na KANSA kwa miezi
kadhaa lakini sikujua kwa sababu nilikuwa
nimetekwa na Jane. Bila mimi kufahamu,
kumbe marehemu mke wangu alijua kwamba
muda si mrefu atafariki dunia na alitaka
kuniokoa dhidi ya fikra yoyote mbaya kutoka
kwa mtoto wetu kama tungeachana muda

kabla ya kifo chake. Angalau machoni mwa
mwanangu naonekana kuwa mume mwenye
upendo WAPENDANAO NATAKA MJIFUNZE
 1) Wengi wanatengana si kwa sababu
hawapendani, bali hawapeani muda wa
kusikilizana.
 2)Wengi wanaamini ukiachana na
mpendwa
wako ni lazima muwe maadui.
 3)Busara ndani
ya pendo ni zaidi ya mali na
pesa......

Previous
Next Post »