Mwamuzi wa kimataifa wa Tanzania mwenye beji ya FIFA, Israel Mjuni Nkongo akiwa kazini
Mwamuzi wa kimataifa wa Tanzania mwenye beji ya FIFA, Israel
Mjuni Nkongo amechaguliwa kuchezesha mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika
(CL) kati ya wenyeji Zesco FC ya Zambia dhidi ya AS Kaloum ya Guinea.
Katika
mchezo huo wa kwanza wa mzunguko wa pili, Nkongo atasaidiwa na washika
kibendera John Kanyenye na Josephat Bulali na mwamuzi wa akiba Waziri
Sheha wote kutoka Tanzania, huku Kamisaa wa mchezo akiwa Mayixole Elvin
Shishana kutoka nchini Afrika Kusini
Mchezo huo unatarajiwa kufanyika kati ya tarehe 13,14,15 Machi mwaka huu nchini Zambia.
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon