Mwanamke anayedaiwa kuwa na sura mbaya duniani na mitandao inayomuonea ametoa filamu kuhusu maisha yake.
Lizzie ambaye alikuwa na
miaka 17 wakati huo alikasirishwa kuona kwamba msichana aliyekuwa katika
kanda hiyo ya video alikuwa yeye.
Kanda hiyo ilioonekana mara
millioni 4 mtandaoni huku wengi wakiwacha ujumbe wa kuudhi kama vile
''angeuliwa alipozaliwa'',nilishangaa nilipoona ujumbe huo alisema
Lizzie.
Ujumbe mwengine ulisoma ''kwa nini wazazi wake walimlea''.
Mwanamke
huyo alipiga moyo konde na kuanza mtandao wake wa You Tube akiwaelezea
watu kuhusu mwanamke huyo anayedaiwa kuwa mwenye sura mbaya zaidi.
Lizzie amesema kuwa anawasaidia wengine ambao wamekuwa wakionewa kuweza kupata msaada ama hata kupambana na maonevu hayo.
Mwanamke huyo pia anafanya kazi na Tina Meir ambaye mwana wao Mega alijiuwa baada ya kuonewa katika mtandao.
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon