SERBIA
ina makocha wa soka zaidi ya 270 na bado wanazidi kuibuka wapya kila
kukicha. Moja kati ya sifa za makocha wa nchi hiyo ni ujanja wa kucheza
na akili za wachezaji ili kutengeneza matokeo.
Wanaujulia mpira wa Kiafrika, wanajua kuigiza hata kuzuga kuendana na mazingira ya sehemu husika ndio maana hawabanduki kirahisi kwenye ardhi ya Afrika.
Mfano
mdogo Kostadin Papic na Sredejovic Milutin ‘Micho’ ambao waliwahi
kuinoa Yanga, ni makocha wenye mbwembwe kuanzia kwa mashabiki mpaka kwa
wachezaji na wanajua kuwajaza upepo wachezaji wapambane kiume hata
katika mazingira ambayo hayawezekani.
Mserbia
wa Simba, Goran Kopunovic, naye yupo hivyo na amefanya kituko kimoja
katika maandalizi yake ya mechi dhidi ya Yanga ya keshokutwa Jumapili
jioni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Unajua amefanya nini? Amefanya jambo ambalo kwa jinsi wachezaji wa Simba wanavyomkubali kwa sasa, hawawezi kukubali litokee.
Kocha
huyo mwenye mkataba wa miezi sita unaomalizika mwisho wa msimu, Jumanne
usiku alizungumza na wachezaji wake mjini hapa na katika moja ya mambo
ya kusikitisha aliyowaambia ni pale alipowaaga kwamba endapo watafungwa
na Yanga basi huenda akatimuliwa.
Mmoja
wa wachezaji wa Simba aliidokeza Mwanaspoti kwamba bosi huyo amewaambia
kwamba anawatakia kila la heri kama ikitokea bahati mbaya wamepoteza
mchezo na yeye akapoteza kazi yake.
Imebainika
kwamba wachezaji wametokea kumkubali kocha huyo hivyo gia aliyotumia ni
kama kuwahamasisha wachezaji wake wajitume na kuifunga Yanga jambo
ambalo lilijionyesha kwenye mazoezi yaliyofanyika juzi Jumatano jioni
ambapo wachezaji walionekana kuwa na morali ya hali ya juu.
“Kocha
katuaga wakati anazungumza na sisi, unajua ana historia ya kufukuzwa
kwa Maximo(Marcio), hivyo anaona kama Maximo alifukuzwa Yanga kwa
kufungwa na sisi, je ikitokea sisi kupoteza mechi hiyo itakuwaje kwake?
Hivyo anaamini pengine na yeye atafukuzwa, tunapambana kuhakikisha Yanga
hawatoki na kumlinda kocha wetu,” alisema mchezaji huyo tegemeo wa
kikosi cha kwanza.
Goran
ambaye amefunga kuzungumza na vyombo vya habari mpaka baada ya mechi
hiyo ya Ligi Kuu Bara, huenda aliaga mapema kutokana na historia
aliyokutana nayo ya kutimuliwa kwa makocha mara tu wanapofungwa na timu
pinzani kama ilivyokuwa kwa Maximo baada ya mechi ya Nani Mtani Jembe
alipokubali kichapo cha mabao 2-0.
Habari
kutoka ndani ya kambi hiyo, zinasema kuwa Goran amekuwa na wasiwasi na
matokeo ya mechi hiyo na kulazimika kuwasisitiza wachezaji wake wacheze
kwa kujituma ili kumlinda asisitishiwe kibarua chake ingawa Mwanaspoti
linajua kwamba uongozi wa Simba una mipango mirefu na Goran.
Goran
alitua Simba baada ya uongozi kusitisha mkataba wa kocha raia wa
Zambia, Patrick Phiri ambaye alishindwa kutimiza malengo kutokana na
timu yao kusuasua kwenye ligi, Phiri alifundisha mechi nane na kati ya
hizo alishinda moja tu na nyingine zote kutoka sare.
Hata
hivyo, Phiri alikutana na Yanga mara mbili ambapo mechi ya Ligi Kuu
Bara walitoka sare ya bila kufungana huku akishinda mechi ya Mtani Jembe
na kufukuzwa baada ya kufungwa na Kagera Sugar bao 1-0.
Wakati
kocha huyo anarudi kwao Zambia alitoa neno moja kwa Goran kuwa ili
ajiwekee imani kubwa kwa wanachama na viongozi wa Simba ni lazima
ashinde mechi yao na Yanga ambayo itachezwa keshokutwa Jumapili.
Kwa
sasa Simba inashika nafasi ya nne kwenye msimammo wa ligi hiyo ikiwa na
pointi 23 wakati Yanga wao wanaongoza wakiwa na pointi 31, jambo ambalo
Simba wametamba kuwa watashinda mechi zao zijazo na kuwasimamisha
Yanga.
MAKOMANDOO SABA
Yanga
ipo Bagamoyo moja ya sehemu tulivu na ni kawaida kwao kuweka kambi
huko, kama Yanga hawajaweka kambi Bagamoyo basi hutimkia Pemba ama
watabaki Dar es Salaam lakini pamoja na hayo habari za ndani zinasema
wametuma makomandoo wao saba kuichunguza Simba inafanya nini visiwani
hapa.
Mratibu
wa Simba ambaye pia ni mjumbe wa kuteuliwa, Abdul Mshangama ameliambia
Mwanaspoti akisema: “Tunawafahamu waliokuja hapa ni akina nani, kikao
chao walikifanya jijini Dar es Salaam na kuwatuma watu wao hapa, kuna
makomandoo watatu na wazee wao wanne lakini kamwe hawatuwezi.”
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon