Mzee
Yussuf anaweza kuwa mfano mzuri sana kwa wanamuziki wengine kwa namna
anavyowekeza ili asitetereke pale atakapoamua kuupa mkono wa kwaheri
muziki au muziki kumpa mkono wa kwaheri.
Mfalme
huyo wa taarab anayemiliki kundi la Jahazi Modern Taarab, ana mradi
mkubwa wa kuuza vifaa vya ujenzi ikiwemo cement na mtofali ya kisasa
huko Chanika na Kigamboni.
Mzee
Yussuf ana viwanja viwili vyenye mradi wa kufyatua matofali huko
Chanika na kimoja kingine Kigamboni. Ni miradi mikubwa ambayo iko chini
ya mwamvuli wa kampuni yake inayojulikana kama M.Y. Contractors.
Katika
kurahisisha kazi za M.Y. Contractors, Mzee Yussuf anamikili malori ya
Scania na Fuso ambayo hutumika kubeba michanga, matofali na vifaa
vingine kwaajili ya viwanda vyake pamoja na wateja wake.
Hakika
Mzee Yussuf yuko vizuri sana kwani Saluti5 ilipotembelea moja ya
viwanja vyake vya Chanika, ikashuhudia ujenzi wa mjengo wa maana
utakaokuwa na gorofa moja kwaajili ya makazi yake na familia yake.
Lakini
ndani ya uwanja huo mkubwa unaoweza kujenga hata nyumba 20 za kawaida,
kuna nyumba nyingine ya maana ambayo nayo ujenzi wake haujakamilika. Ni
nyumba mbili za maana kwa mpigo, achalia mbali jengo lenye maduka na
ofisi yake.
Katika
kuonyesha kuwa kiwanja hicho ni kikubwa kupindukia, sehemu ya mbele
Mzee Yussuf amejenga jengo lenye maduka manne ambayo yote yatahusiana na
kazi za M.Y. Contractors lakini pia nyuma ya maduka hayo kuna vyumba
vingine ambavyo vitatumika kama ofisi yake na maafisa wengine wa
kampuni.
Mzee
Yussuf ameidokeza Saluti5 kuwa ameanzisha pia mradi mkubwa wa kufuga
kuku wa nyama na mayai (wa kisasa na kienyeji) huko Kigamboni.
Kwa namna alivyowekeza Mzee Yussuf, hakuna ubishi kuwa nyota huyo sasa anaweza kabisa kuishi bila kutegemea pato la muziki.
Jengo lenye maduka likiwa kwenye hatua za mwisho za ujenzi
Hapa kutakuwa na maduka ya vifaa vya ujenzi na magari
Uwanja wa Mzee Yussuf unavyoonekana kwa mbele
Mama muuza samaki ni akifanya biashara yake ndani ya uwanja wa Mzee Yussuf, ujirani uliotukuka!
Mzee Yussuf akimuunga mkono jirani yake
Mzee Yussuf akiangalia namna kazi zinavyoendelea
Sehemu ya mradi wa matofali inavyoonekana
Sehemu ya pili ya mradi wa matofali
Baadhi ya vitendea kazi
Hii ni nyumba mpya ya Mzee Yussuf inavyoonekana kwa nyuma
Nyumba mpya ya Mzee Yussuf inavyoonekana kwa ubavuni
Inavyoonekana kwa mbele
Sehemu ya mbele kwa karibu zaidi
Si mjengo wa kitoto!
Mzee Yussuf mbele ya mjengo wake
Hii ni nyumba nyingine ya Mzee Yussuf ambayo ipo kwenye uwanja wake huo huo wa Chanika
Huu nao ni mjengo wa haja
Jengo lenye maduka linavyoonekana kwa nyuma
Mzee Yussuf akifurahia upepe mwanana wa Chanika
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon