Wakati kamatakamata ya waganga wa kienyeji ikiendelea kupamba moto katika mikoa ya Kanda ya Ziwa, mmoja amenaswa akiwa na viungo vya binadamu, kikiwemo kichwa ambacho bado kilikuwa na nywele zake.
Mganga huyo,
Nyamizi Makunga (70), mkazi wa Kijiji cha Igurubi wilayani Igunga,
Tabora, alitiwa mbaroni juzi. Mbali na viungo hivyo, pia alikutwa na
vifaa vingine, zikiwemo nyara za serikali.
Mwenyekiti wa
Kijiji cha Igurubi, George Henry, alisema Makunga alikamatwa nyumbani
kwake kutokana na msako mkali unaendelea kwa lengo la kuwabaini waganga
wanaofanya ramli chonganishi.
Msako huo
umetokana na kukithiri kwa mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi, ambapo
serikali katika kubaini chanzo, imekuwa ikisaka waganga wanaotuhumiwa
kufanya ramli hizo.
Henry alisema
polisi walifanikiwa kumnasa Makunga kutokana na taarifa kutoka kwa raia
wema, ambapo walipofanya msako walikuta fuvu la kichwa la binadamu
likiwa na nywele zake.
Mbali na fuvu
hilo, polisi pia walikuta kipande cha mfupa wa binadamu, mkia wa nyumbu,
gamba la kobe na ngozi za wanyama mbalimbali.
Wananchi wa
Kijiji cha Igurubi, wamepongeza msako unaofanywa na polisi kuwatia
mbaroni waganga ambao ndio chanzo cha kushamiri kwa mauaji ya albino.
Pia walisema
kwa muda mrefu Makunga amekuwa kikwazo cha maendeleo kwenye eneo hilo
kutokana na kufanya mambo kinyume na kwamba wananchi wamekuwa
wakimwogopa.
Alipohojiwa, Makunga alikiri viungo hivyo ni vya binadamu na kuwa aliachiwa na baba yake ili kuendesha shughuli za uganga.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Suzana Kaganda, alithibitisha kukamatwa kwa mganga huyo akiwa na viungo vya binadamu.
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon