MAMBO
hadharani! Supastaa wa Bongo, Wema Sepetu ‘madam’ ameanika siri
zilizojificha nyuma ya pazia kati yake na aliyekuwa mume wa mwanamuziki
nyota wa Uganda, Zarina Hassan ‘Zari’, Ivan Semwanga, kuwa anataka
kumuoa, Risasi Jumamosi lina full stori.
Supastaa wa Bongo Movie, Wema Sepetu ‘madam’.
WALIANZIA KUKUTANA SAUZ Katika
mazungumzo yake exclusive na mwanahabari wetu juzi jijini Dar, Wema
alianza kwa kuweka bayana kwamba, mawasiliano yake na Ivan yalianzia
nchini Afrika Kusini wakati alipokwenda kikazi, Februari, mwaka huu.
“Nilikwenda
na Ommy Dimpoz (Faraj Nyembo). Tulikuwa na project yake lakini
tulipokuwa kule, Ivan na marafiki zake walisikia kuwa mimi nipo,
wakatuomba sana kupitia kwa wenyeji wetu kuwa wanataka kutuona na kutoka
nao out pamoja.”
ALIBANA, AKALEGEZA “Mimi
nilikuwa bize sana na kazi zangu, awali niliwaambia kuwa hatutaweza
lakini baadaye walitubahatisha klabu, wakaomba kukaa na sisi, mwishoni
ilibidi tuwakubalie lakini kwa masharti ya kuwa wasije wakatuzushia
lolote.
“Tulikubali,
wakaja, tukakaa nao meza moja, tukabadilishana mawasiliano kama
marafiki. Lakini baadaye tukaona wanaongezeka, sikupenda vurugu ya watu
wengi, mimi na Ommy tukaamua kuondoka zetu,” alisema Wema.
IVAN AANZA ‘KUIMBISHA’ Akizidi
kumwaga siri zake na mwanaume huyo, Wema alisema baada ya yeye kumaliza
project yake nchini humo, alirejea Bongo na ndipo Ivan alipozidisha
ufundi wa kumuomba urafiki wa kimapenzi huku akimuahidi mambo mengi ya
muhimu.
Msikie
Wema: “Baada ya hapo tulikuwa tunawasiliana na Ivan, lakini kadiri siku
zilivyokuwa zikisonga mbele, nikaona mwenzangu anaanza kunitongoza, tena
akawa anaendelea kila siku licha ya mimi kutomkubalia.”
Aliyekuwa mume wa mwanamuziki nyota wa Uganda, Zarina Hassan ‘Zari’, Ivan Semwanga.
AHADI NI MAGARI, NYUMBA Wema
alizidi kutiririka kuwa, hadi sasa (mapema wiki hii), Ivan hajakata
tamaa, amekuwa akiendelea kumtongoza na kumuahidi ahadi mbalimbali. Endapo atamkubalia na kuwa baby wake, basi atampa nyumba ya kifahari na magari ya kisasa (awe kama Zari).
Wema
anakiri mwenyewe: “Alianza kuniahidi maisha mazuri, nyumba, magari na
hata kunioa lakini kimsingi sijamkubalia kwani sijamwamini kama ana
mapenzi ya dhati. Nahisi kuna kitu nyuma yake kinamsukuma kufanya
hivyo.”
ATAKIWA KUTOICHEZEA BAHATI Kwa
mujibu wa chanzo makini, kuna uwezekano mkubwa Wema akaingia kwenye
himaya ya Ivan kutokana na ushawishi wake mkubwa anaoufanya kwa madam
huyo, hivyo akawa tajiri mkubwa. “Wema
kwa sasa hatakiwi kuichezea bahati kwani Ivan ni mtu anayejiheshimu.
Ana biashara zake kubwakubwa, hivyo suala la fedha za maisha hazimpigi
chenga,” kilisema chanzo hicho.
WEMA KUWA KAMA MCHARO? Akizungumzia
suala hilo, rafiki wa karibu wa Wema ambaye hakupenda jina lake
liandikwe gazetini, alisema licha ya Wema kutokubali ombi la Ivan lakini
anaamini siku si nyingi atakubali na atakuwa vizuri kiuchumi kuliko
alivyo sasa.
“Jamaa yupo
serious na ndoa, Wema atakubali tu na ndoa itafungwa. Mtoto wa kike
sasa atakuwa si wa magari ya kawaida, full kubadilisha, atakuwa mtamu
kama mcharo,” alisema rafiki huyo.
KINACHOMPA WASIWASI WEMA Rafiki
huyo aliendelea kusema kuwa, Wema ana wasiwasi kwamba, mapenzi ya Ivan
kwake ni kwa ajili ya kulipa kisasi kwa sababu ya Diamond (aliyekuwa
mpenzi wa Wema) sasa yuko na Zari (aliyekuwa mke wa Ivan).
“Kwa hiyo
Wema ana wasiwasi kwamba, siku akimkubalia tu Ivan akapiga naye ngwara,
biashara itakuwa imeishia hapo kwani nia ya kisasi ya mwanaume huyo
itakuwa imekamilika,” alisema rafiki huyo
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon