Chid Benz alikiri hivyo jana Jumatano
mbele ya Hakimu Mkazi, Waliarwande Lema baada ya kuomba asomewe tena
mashtaka yake. Aliomba hivyo muda mfupi baada ya kesi yake kutajwa
mahakamani hapo na Wakili wa Serikali, Diana Lukendo aliyesema upelelezi
haujakamilika hivyo kuomba ipangiwe tarehe nyingine
MWANAMUZIKI Chid Benz (29), amekiri mashtaka
matatu yanayomkabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es
Salaam ya kukutwa na dawa za kulevya, kifuu cha nazi na kijiko
vinavyotumika kuvutia ama kunusa dawa hizo.
Chid Benz alikiri hivyo jana Jumatano mbele ya
Hakimu Mkazi, Waliarwande Lema baada ya kuomba asomewe tena mashtaka
yake. Aliomba hivyo muda mfupi baada ya kesi yake kutajwa mahakamani
hapo na Wakili wa Serikali, Diana Lukendo aliyesema upelelezi
haujakamilika hivyo kuomba ipangiwe tarehe nyingine.
Baada ya maelezo hayo, Chid Benz alinyoosha mkono
na kuiomba mahakama imsomee tena mashtaka yanayomkabili, akasomewa na
kukiri kuwa Oktoba 24,2014 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Mwalimu Julius Nyerere alikamatwa na gramu 0.85 za Heroin Hydrochloride
zenye thamani ya Sh38,638.
Alikiri pia alikutwa na gramu 1.72 za bangi zenye
thamani ya Sh1720 na vifaa vinavyounganishwa na matumizi ya kuvuta ama
kunusa dawa hizo.
Baada ya kukiri mashtaka hayo yote matatu, Wakili
wa Serikali, Lukendo aliiomba mahakama kutoa ahirisho fupi ili waweze
kujiandaa na kumsomea maelezo ya makosa yanayomkabili. Hakimu Lema
alikubaliana na ombi hilo na kuiahirisha kesi hadi Februari 23, 2015.
Awali kesi hiyo ilipotajwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo, Chid Benz aliposomewa mashtaka hayo aliyakana yote.
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon