Di Maria aichanganya Manchester United

MANCHESTER United inakesha ikiomba Mungu ukakamavu wa Angel di Maria urejee katika hali yake ya kawaida baada ya kiungo huyo kuumia wakati wa mazoezi juzi Jumanne.
Habari kutoka klabuni hapo zinasema staa huyo wa kimataifa wa Argentina alipatiwa matibabu ya awali uwanjani hapo, lakini ameibua hofu kwamba huenda akawa ametonesha nyonga, tatizo lililomweka nje ya uwanja wakati wa Krismas


     style="display:inline-block;width:680px;height:300px"
     data-ad-client="ca-pub-3992075039970891"
     data-ad-slot="7646462965">

Kutoka na wasiwasi huo, Di Maria anaweza kupumzishwa kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi zaidi.
Kikosi hicho cha kocha, Louis van Gaal, Jumamosi kitakuwa na mechi ya ugenini dhidi ya Swansea City na uwezekano wa staa huyo kucheza upo mashakani kutokana na hali hiyo.
Nyota huyo wa zamani wa Real Madrid aliyeianza Ligi Kuu England kwa kasi alipofunga mabao matatu na kusababisha mengine manne katika mechi sita za awali, katika miezi ya karibuni amekuwa na wakati mgumu akifunga mara moja tu katika michezo 16.
Kuumia kwa Di Maria kunaongeza hofu kwa kocha Mholanzi Van Gaal hasa kwa kuwa Phil Jones na Michael Carrick nao pia wapo katika benchi la majeruhi. Hata hivyo, kocha huyo anapumua kutokana na habari kuwa straika, Robin van Persie, amepona matatizo yake yaliyomkosesha mechi ya Kombe la FA dhidi ya Preston North End na anatarajiwa kuivaa Swansea
Previous
Next Post »