Mwenyekiti
wa Kamati ya kuendeleza ujenzi wa Misikiti na Madrasa Zanzibar Rais
Mstafu wa Tanzania Al-Hajj Ali Hassan Mwinyi akitoa salamu wakati wa
hafla ya ufunguzi wa Msikiti Mpya wa Ijumaa wa Kijiji cha Bandamaji
Mvumoni Mkoa wa Kaskazini Unguja.Kulia
ya Mzee Mwinyi ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali
Iddi na Mfadhili wa Ujen zi wa Msikiti huo Sheikh Muhoma.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na waumini
wa dini ya Kiislamu wa Kijiji cha Bandamaji Mvumoni mara baada ya
kuufunguwa rasmi Msikiti wa Ijumaa wa Kijiji hicho kwa niaba ya Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Al-Hajj Dr. Ali Mohammed
Shein.
Balozi
Seif akigawa Misahafu kwa ajili na Madrasat Taawun na Masjid Bilal wa
Kijiji cha Bandamaji Mvumoni mara baadsa ya kuzindua Msikiti na Madrasa
hiyo kwa niaba ya Rais wa Zanzibar.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akibadilishana mawazo
na Mke wa Mfadhili wa Ujenzi wa Msikiti Bilal wa Bandamaji Mama Fatma
nje ya msikiti huo.Kati kati yao ni Mjumbe wa Baraza la Ulamaa Mkoa wa Kaskazini Unguja Sheikh Khamis Abdulhamid.(Picha na –OMPR )
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon